Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:10

Wanajeshi 10 wauawa katika shambulizi Burkina Faso


Wanajeshi wa Burkina Faso.
Wanajeshi wa Burkina Faso.

Takriban wanajeshi 10 wa Burkina Faso waliuawa na karibu 50 kujeruhiwa Jumatatu katika shambulio kwenye mji wa kaskazini wa Djibo, jeshi lilisema.

Chanzo cha kitengo cha usalama kililiambia shirika la habari la AFP kwamba washambuliaji hao walirusha vilipuzi kwenye kambi hiyo ya Djibo.

Jeshi liliongeza kwamba angalau mili 18 ya magaidi ilihesabiwa wakati wa operesheni ya kuwaondoa.

Kwa miezi mitatu sasa, idadi kubwa ya wakazi wa Djibo, wasiopungua 30,000, imetengwa kutoka kwa maeneo mengine ya nchi, huku wanajihadi wakidhibiti barabara kuu baada ya kulipua madaraja.

Shambulio dhidi ya msafara wa usambazaji bidhaa uliokuwa ukielekea Djibo tarehe 26 mwezi jana, lilisababisha vifo vya watu 37, 27 kati yao wakiwa wanajeshi.

Madereva sabini wa malori bado hawajapatikana. Shambulio hilo lilichochea mapinduzi ya hivi punde nchini Burkina Faso, siku nne tu baadaye, yakiongozwa na Ibrahim Traore.

Yalikuwa ni mapinduzi ya pili ya taifa hilo la Afrika Magharibi katika kipindi cha miezi minane.

XS
SM
MD
LG