Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 17:36

Wanaharakati wa Sudan Kusini wameandamana Washington DC


Baadhi ya waandamanaji wa Sudan Kusini wakiwa White House, April 16, 2018.

Darzeni kadhaa ya waandamanaji wa Sudan Kusini na wanaharakati wa kisiasa baadhi yao wakiwa ni wafuasi wa chama cha upinzani cha SPLM-IO walikusanyika mbele ya White House siku ya Jumatatu wakipinga kuendelea kwa vita katika nchi yao ya asili.

Takriban waandamanaji 25 walipiga kelele wakisema “Watu wa Sudan Kusini wanakufa” na “tunahitaji amani nchini Sudan Kusini”.

Akiongea kwa lugha ya kiarabu, Elizabeth James, muandamanaji kutoka Tennessee, alisema muda unakwenda wa kuchukua hatua kwa Sudan Kusini. “Tukiacha huu mpango wa kutafuta amani uwe kwenye mikono ya serikali na waasi,’ alisema. ‘Watachukua muda wao kwa sababu ya maslahi yao binafsi”.

James aliendesha gari kwa saa tisa kuhakikisha anashiriki maandamano ya Jumatatu akisema ilikuwa ni wajibu wake kutoa sauti kuelezea wasi wasi wake. “Wako wapi raia wa Sudan Kusini? Kila siku tunafariki, kila siku tuna njaa, kila siku tumetawanyika, kila siku tunakwenda katika nchi nyingine” James alisema.

Waandamanaji wa Sudan Kusini wakiwa Washington DC. April 16, 2018.
Waandamanaji wa Sudan Kusini wakiwa Washington DC. April 16, 2018.

Waandamanaji walishika mabango na kuvaa mashati yaliyoandikwa “Rais Trump ataifanya Sudan Kusini iwe nzuri tena” wakati mabango mengine yalilenga biashara ya Afrika, Mamlaka ya Maendeleo ya Kikanda-IGAD bango lililosomeka “IGAD imeshindwa na imejaa rushwa kiasi cha kushindwa kuleta amani Sudan Kusini”.

Isaac Gang, mwakilishi wa chama cha upinzani nchini Marekani na muaandaaji wa maandamano, alisema IGAD ina fursa ya kubadili mambo wakati wakiandaa mazungumzo yajayo ya amani. “Kwa kweli naamini kama wadau nchini Sudan Kusini watachukua fursa ya kufufua mkutano wa ngazi ya juu kuna jambo zuri linaweza kutokea” alisema Gang. “Lakini kama tukirejea kwenye usingizi wa kawaida watu watatumia fursa kama hii kupoteza muda kinyume na kutumia fursa kama hii kuleta Amani”.

Mazungumzo yanatarajiwa kufanyika katika wiki chache zijazo kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

XS
SM
MD
LG