Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 23, 2025 Local time: 23:13

Wanafunzi wa Florida wapanga maandamano DC na kwingineko


Wanafunzi wa shule huko Florida wakiandamana kupinga mauaji ya bunduki
Wanafunzi wa shule huko Florida wakiandamana kupinga mauaji ya bunduki

Wanafunzi walionusurika na mauwaji katika shule ya sekondari Marjory Stoneman Douglas huko Florida nchini Marekani wametangaza maandamano mjini Washington na miji mingine muhimu ya Marekani mwezi ujao ili kudai hatua thabiti zaidi zichukuliwa kuzuia mauwaji mengine kuweza kutokea katika shule za nchini Marekani.

Cameroon Kasey mwanafunzi wa shule ya sekondari alikiambia kipindi cha “This week” cha kituo cha televisheni cha ABC kwamba “tutaandamana pamoja kama wanafunzi ili kuwa aibisha wanasiasa wanaokubali kupokea fedha kutoka chama cha wamiliki bunduki Marekani-NRA. Na tutataka maisha yetu yalindwe.”

Alizsema NRA inahamasisha mila ya umiliki bunduki inayosababisha maafa haya yote.

Mwanafunzi mwingine Emma Gonzalez ameiambia ABC kwamba Rais Trump, Seneta Marco Rubio wa jimbo la Florida na gavana wa jimbo lao Rick Scott wanaunga mkono NRA.Gonzalez alisema hawatakwenda katika kikao cha Rais Trump siku ya Jumatano.

Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

White House imetangaza kwamba Rais Trump atakutana na wanafunzi pamoja na walimu wao katika kikao cha kusikiliza madai yao lakini White House haikutoa maelezo zaidi juu ya kikao hicho.

XS
SM
MD
LG