Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 16:50

Wanadiplomasia wa Uganda warudishwa nyumbani


Rais Yoweri Museveni wa Uganda

Uganda inawarudisha nyumbani wanadiplomasia wake wanaohusishwa na kashfa ya kupanga kugawana fedha za umma kuvuja katika mazungumzo yao yaliokuwa yamerikodiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imewaamrisha kurudi nyumbani wanadiplomasia hao waliokuwa katika ubalozi wa nchi hiyo nchini Denmark ili kuwezesha uchunguzi kufanyika, amesema Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Patrick Mugoya katika tamko lake Jumatatu.

Ameeleza kuwa Mkaguzi Mkuu wa serikali atafanya “uchunguzi wa kina juu ya kashfa hiyo.”

Hatua zitakazo chukuliwa amesema Mugoya “Zitategemea na matokeo ya uchunguzi huo na hatua nyingine stahiki zaidi zitachukuliwa.”

Katika sauti zilizorikodiwa katika mazungumzo ya mtandao wa Zoom, na kuripotiwa na mtandao wa habari wa ChimpReports, Balozi Nimisha Madhvani, naibu wake, Elly Kamahungye Kafeero na wafanyakazi wengine wanasikika wakibadilishana mawazo jinsi ya kutumia fedha ambazo ziliainishwa kwa ajili ya matayarisho ya COVID-19.

Mfanyakazi katika ubalozi huo anauliza kiasi gani kigawiwe kwa wanadiplomasia hao.

Kamahungye baadaye katika mazungumzo hayo anapendekeza “siku nane.”

Nimisha anaendelea kuuliza, “siku nane – kwa kila mtu, uh?”

Kamahungye anajibu : Jigawieni kila mmoja (dola) 4000.”

Bado haijafahamika nani aliyerikodi mazungumzo hayo. Lakini, inawezekana kuwa mmoja wa wafanyakazi wa ubalozi alifanya hivyo.

Mmoja wa wanadiplomasia hao mwanamke anasikika akilalamika katika mgao huo wenye wasiwasi, wengine wanapata zaidi kuliko sisi.”

Kamahungye anajibu : Nyinyi ndio mlioweka fedha hizi.”

Katika hali ya kusitushwa, Nimisha anasikika akimwambia Kamahungye kuwa “ ikiwa kuna kiwango chochote kimebakia” fedha hizo “azitafutie njia ya kuzitumia.”

Pia mwanamke huyo anapendekeza kuwa katika kugawana fedha hizo, wafanyakazi wa ngazi ya chini na maafisa usalama waambata wa ubalozi wasipewe taarifa hizi za mgao huu.

Mugoya alisema Wizara haiwezi kuendeleza ufisadi na kuwa, matumizi ya fedha hizo za umma yatafuata misingi ya uwazi na ufanisi na kitendo chochote cha ofisa yeyote kukiuka utaratibu huo adhabu kama inayoonyeshwa katika Sheria ya Fedha za Umma na Utawala zitatolewa kwa atakaye kwenda kinyume.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG