Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:22

Mafuriko Uturuki yaua watu 4, wengine 11 hawajulikani waliko


Harakati za uokoaji zikiendelea nchini Uturuki baada y mvua zilizosababisha mafuriko katika mkoa wa Giresun Turkey.
Harakati za uokoaji zikiendelea nchini Uturuki baada y mvua zilizosababisha mafuriko katika mkoa wa Giresun Turkey.

Watu wasiopungua wanne wamekufa na wengine 11 hawajulikani waliko baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko katika pwani ya bahari ya Black Sea Uturuki.

Waziri wa Mambo ya Ndani Suleyman Soylu akizungumzia mafuriko hayo amesema Jumapili kati ya waliofariki mmoja wao ni afisa wa polisi ambaye gari lake lilisombwa na maji.

Akitembelea mji wa Dereli, katika mkoa wa Giresun, Soylu alisema watu 127 wameokolewa na kuwa barabara zinazoelekea katika vijiji 118 katika eneo hilo la mafuriko zimefungwa.

Picha za Televisheni zilionyesha magari na vifusi vikielea katika barabara kuu ya Dereli iliyoko takriban kilomita 20 kutoka pwani.

Mvua kubwa Jumamosi jioni ililazimisha kuokolewa watu katika nyumba za ghorofa baada ya maporomokoya ardhi kutokea katika mkoa wa Rize, kilomita 180 mashariki ya Giresun.

Kwa mujibu wa Kituo cha kutabiri hali ya hewa, mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha huko Giresun na mikoa iliyoko jirani ya Trabzon, Rize na Artvin lat.

XS
SM
MD
LG