Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 10:02

ECOWAS na viongozi wa mapinduzi Mali wafikia makubaliano


Ujumbe wa ECOWAS ukiongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan uliwasili Mali Jumamosi.
Ujumbe wa ECOWAS ukiongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan uliwasili Mali Jumamosi.

Wapatanishi wa Jumuia ya uchumi ya Africa Magharibi Ecowas  na viongozi wa mapinduzi wa Mali wamekubaliana juu ya  baadhi ya mambo yanayolenga kurejesha utawala wa kiraiya baada ya mapinduzi ya wiki iliyopita yaliomuondoa madarakani rais Ibrahim Boubacar Keita.

Wajumbe wa pande zote mbili wanaendelea na mazungumzo yao leo kwa siku ya tatu mfululizo mjini Bamako ikisemekana wanajeshi wanataka kubaki madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mazungumzo yanaendelea Jumatatu, pande hizo zimewaambia waandishi wa habari.

Viongozi wa kijeshi wanaongozwa na Kanali Assimi Goita na wasuluhishi wa ECOWAS wanaongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan walikutana jana katika kikao cha faragha.

Mazungumzo kati ya ECOWAS na viongozi wa Mapinduzi Mali yaendelea
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:40 0:00

Msemaji wa kundi la wanajeshi kanali Ismael Wague nae amesema wamekubaliana kuhusu baadhi ya maswala na mashauriano zaidi yataendelea.

Maswala nyeti yanazongumziwa ni pamoja na hatma ya rais aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacar Keita na maelezo kuhusu utawala wa mpito kukabidhi madaraka kwa serekali ya kiraia.

Radio Ufaransa RFI, Jumapili usiku ilisema kundi la kijeshi limependeleza serikali ya mpito ya miaka mitatu inayongozwa na mwanajeshi na ambayo inaundwa na wanajeshi wengi.

Taarifa hiyo ya RFI imeongeza kuwa wanajeshi wako tayari kumuruhusu Keita kurudi nyumbani kwake au kuondoka nchini.

XS
SM
MD
LG