Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 10:03

Ujumbe wa ECOWAS wawasili Mali kukutana na viongozi wa mapinduzi

Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan (katikati) akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bamako alipowasili Agosti 22, 2020, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kimataifa kutafuta suluhu juu ya mgogoro wa Mali baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Ujumbe maalum wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, ukiongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan umewasili mjini Bamako, Mali kukutana na viongozi wa baraza la kijeshi lililomlazimisha Rais Ibrahim Boubacar Keita kuachia madaraka na serikali yake mapema wiki hii.

Ujumbe wa ECOWAS pia utakutana na rais aliyeondolewa madarakani, Keita, pamoja na maafisa wa serikali na jeshi wanaozuiliwa na wanajeshi waasi, afisa mmoja wa ECOWAS ameliambia Shirika la Habari la AFP.

Viongozi hao watakutana na mabalozi wa mataifa matano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wanaotarajiwa kuwasili Bamako siku ya Jumapili.

Ujumbe huo umewasili siku moja baada ya maelfu ya wananchi kumiminika katika mji mkuu wa Mali wakionyesha kuunga mkono baraza hilo la jeshi liliofanya mapinduzi.

Waandamanaji huko Bamako – wengine wakinyanyua mabango yao wakipaza sauti kuwa Kamati ya Kitaifa ni Mkombozi wa Wananchi, CNSP, ni jina ililopewa baraza la utawala wa kijeshi.

Raia wa Mali wanaounga mkono kuondolewa kwa Rais Ibrahim Boubacar Keita wakisheherekea mapinduzi mjini Bamako, Mali, Agosti. 21, 2020.
Raia wa Mali wanaounga mkono kuondolewa kwa Rais Ibrahim Boubacar Keita wakisheherekea mapinduzi mjini Bamako, Mali, Agosti. 21, 2020.

Waandamanaji vile vile wanapinga ECOWAS kwa tamko lao la kulaani mapinduzi hayo na kwa kufunga mipaka ya majirani wa nchi ya Mali katika umoja wa eneo lenye nchi 14 wanachama.

Viongozi wa kijeshi waliofanya mapinduzi wamesema Ijumaa wamefungua mipaka kwa safari za anga na ardhini.

XS
SM
MD
LG