Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 21:45

Wanadiplomasia na raia wa nchi za nje waondolewa Khartoum


Msafara wa magari ukiondoka Khartoum kuelekea bandari ya Sudan, Aprili 23, 2023. Picha na Abubakarr JALLOH /AFP.
Msafara wa magari ukiondoka Khartoum kuelekea bandari ya Sudan, Aprili 23, 2023. Picha na Abubakarr JALLOH /AFP.

Nchi zinaharakisha kuwaondoa wanadiplomasia na raia wao kutoka Khartoum, mji mkuu wa Sudan, wakati mapigano yakiendelea kati ya pande mbili hasimu katika nchi hiyo ya Kaskazini-Mashariki mwa Afrika.

Canada, Misri, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Sweden na Marekani ni miongoni mwa mataifa yanayotumia ndege na misafara kuwaondoa raia wa kigeni kutoka Sudan.

Hadi sasa zaidi ya watu 420 wameuawa, na maelfu wamejeruhiwa.

Raia wa Sudan wanahangaika kujikimu huku umeme ukiwa umekatika na huduma za mtandao wa internet hazipatikani.

Baadhi ya raia wa Sudan wamefanya uamuzi wa kutoroka kwa magari na mabasi kwenye barabara hizo hatari.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema Jumatatu kuwa Umoja wa Mataifa hauondoki Sudan, lakini umewahamisha kwa muda "mamia" ya wafanyakazi katika meneo yaliyopo ndani na nje ya nchi.

Umoja wa Mataifa una takriban wafanyakazi 800 wa kimataifa nchini humo, na wengi wao wako na familia zao mjini Khartoum. Pia kuna takriban raia 3,200 wa Sudan wanaofanyakazi katika umoja huo.

Samantha Power, mkuu wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa, alitangaza Jumapili kuwa shirika hilo limepeleka timu ya wataalam wa kukabiliana na majanga nchini Sudan. Alisema timu awali itakuwa ikifanyika kutokea Kenya.

XS
SM
MD
LG