Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 15:14

Mataifa mengi ya kigeni yameanza kuwaondoa raia wao nchini Sudan


Moshi watanda angani mjini Khartoum, wakati wa mapigano ya Jumamosi April 22, 2023.
Moshi watanda angani mjini Khartoum, wakati wa mapigano ya Jumamosi April 22, 2023.

Majeshi ya Marekani na Uingereza yamewaondoa wafanyakazi wa balozi zao nchini Sudan, huku mataifa mengine yakiharakisha kuwaondoa raia wao na kuwapeleka mahali salama wakati makundi hasimu ya kijeshi yalipambana katika mji mkuu Khartoum Jumapili.

Kuzuka kwa mapigano siku nane zilizopita kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF) kulisababisha mzozo wa kibinadamu, na kuua watu 420 na mamilioni ya raia wa Sudan wakiwa wamekwama wakiwa hawana fursa za huduma za msingi.

Wakati watu wanajaribu kukimbia machafuko, nchi zimeanza kupeleka ndege zao na kuandaa misafara mjini Khartoum ili kuwaondoa raia wao. Baadhi ya raia wa kigeni walijeruhiwa.

Mwandishi wa Reuters amesema milio ya risasi ilisikika kote mjini humo na moshi mweusi umetanda angani.

Pande zinazozozana zimeshtumiana kwa kuushambulia msafara wa Ufaransa, kila upande ukisema raia mmoja wa Ufaransa alijeruhiwa. Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ambayo awali ilisema ilikuwa inawaondoa wafanyakazi wa ubalozi na raia wake, haikutoa maoni yoyote.

Ufaransa imesema ndege ya Ufaransa iliyokuwa imebeba watu 100 ukiwemo ujumbe wa Umoja wa Ulaya mjini Khartoum pamoja na raia wengine iliondoka kuelekea Djibouti, na ndege ya pili iliyokuwa na idadi kama hiyo ilitarajiwa kuondoka muda mfupi baadaye.

Juhudi za kuwaondoa wakazi wa kigeni zimewakasirisha baadhi ya Wasudan ambao wamehisi kuwa pande hasimu zimeonyesha kuwa hazijali usalama wa wenyeji.

XS
SM
MD
LG