Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 05, 2024 Local time: 08:51

Mapambano makali yaifunika Eid al-Fitr nchini Sudan


Waumini wa Kiislamu wakiadhimisha sikukuu ya Eid al-Fitr huko Khartoum tarehe 21 Aprili 21, 2023. Picha na AFP.
Waumini wa Kiislamu wakiadhimisha sikukuu ya Eid al-Fitr huko Khartoum tarehe 21 Aprili 21, 2023. Picha na AFP.

Vikosi vya majenerali wawili hasimu vimepigana vita vikali katika mapambano ya mitaani kwenye mji mkuu wa Sudan siku ya Ijumaa, mashahidi waliripoti, huku pande zote katika mzozo huo wa wiki nzima wakipuuza ombi la sitisho la mapigano kwa kipindi cha kumalizika kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Zaidi ya watu 400 wameuawa na maelfu wamejeruhiwa tangu mapigano yalipozuka Jumamosi kati ya vikosi vinavyomtii mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake, Mohamed Hamdan Daglo, kamanda wa kikosi chenye nguvu cha kijeshi cha Rapid Support Forces (RSF) ambaye ni maarufu kwa jina la Hemet.

Khartoum imetikiswa na milipuko na mapambano kwa usiku wa siku sita mfululizo, madaktari walisema, hata wakati sherehe za Eid al-Fitr zanazo adhimisha kumalizika kwa mwezi mtukufu kwa waislamu waliokuwa wamefunga.

Wanajeshi na wanamgambo walipambana vikali mitaani katika wilaya zenye watu wengi za mji mkuu huo, wakati mashahidi wakiripoti mabomu yalidondoka jirani na makao makuu ya jeshi katika jiji lenye wakaazi milioni tano.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken wametoa wito katika nyakati tofauti za kutaka kusitishwa kwa mapigano kwa "angalau" siku tatu ili kuadhimisha sikukuu ya Eid.

RSF, kikosi chenye nguvu kilichoundwa na wanamgambo wa Janjaweed ambao waliongoza miaka mingi ya ghasia kali katika eneo la mkowa magharibi wa Darfur, walisema waaweka nia ya dhatoi kwa sitisho la mapigano kwa saa 72 kuanzia alfajiri.

Lakini, kama ilivyokuwa katika juhudi za awali zilizotangazwa kufeli kutekeleza sitisho hilo kwa saa 24, kumekuwa na milio ya risasi iliyosikika mitaani huku moshi mweusi ukiwa umetana angani.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG