Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden, ambaye anajulikana katika duru za siasa za Washington kwa karibu nusu karne, ametajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais Marekani na anatarajiwa kuapishwa Januari 20, na kuwa rais mwenye umri mkubwa kuliko marais wote waliopita.
#VOAElections2020 : Wamarekani washeherekea ushindi wa Rais mteule Biden
Wafuasi wa chama cha Demokratik wafurahia tangazo la vyombo vya habari kwamba mgombea kiti cha rais wa chama cha Democratic Joe Biden atakuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2020. Huku wafuasi wa Donald Trump wakiandamana kupinga ushindi huo.

1
Wafuasi wa chama cha Demokratik wakisheherekea baada ya Joe Biden baada ya kutajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais Marekani, Jumamosi, Nov. 7, 2020 mjini Washington. (AP Photo/Manuel Balce Ceneta)

2
Wafuasi wakisheherekea mjini Milwaukee, jimboni Wisconsin, baada ya Joe Biden kutajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais Marekani, Jumamosi, Nov. 7, 2020 Nov. 7, 2020, .

3
Wafuasi wa Rais Donald Trump wakishiriki kwenye maandamano ya "Komesha Wizi" baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa kwamba mgombea Joe Biden ametajwa atakuwa rais, mbele ya bunge la jimbo la Arizona, Phoenix, Marekani Novemba 7, 2020.

4
Wafuasi wa Rais Donald Trump wamekusanyika nje ya bunge la jimbo la Arizona mjini Phoenix Jumamosi, Nov. 7, 2020.