Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden, ambaye anajulikana katika duru za siasa za Washington kwa karibu nusu karne, ametajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais Marekani na anatarajiwa kuapishwa Januari 20, na kuwa rais mwenye umri mkubwa kuliko marais wote waliopita.
#VOAElections2020 : Wamarekani washeherekea ushindi wa Rais mteule Biden
Wafuasi wa chama cha Demokratik wafurahia tangazo la vyombo vya habari kwamba mgombea kiti cha rais wa chama cha Democratic Joe Biden atakuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2020. Huku wafuasi wa Donald Trump wakiandamana kupinga ushindi huo.
5
Watu wakisheherekea katika eneo la jirani la Manhattan, jijini New York wakati vyombo vya habari vikitangaza kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokratik Joe Biden ametajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais, Marekani, November 7, 2020. REUTERS/Andrew Kelly.
6
Rais wa Marekani Donald Trump akicheza golf katika Klabu ya Taifa ya Golf ya Trump huko Sterling, Virginia, Marekani, Novemba 7, 2020, baada ya matokeo ya urais kutangazwa yakimtaja Joe Biden kwamba atakuwa mshindi wa urais.
7
Marianne Hoenow wa jimbo la Connecticut akishangilia ushindi wa Rais mteule Joe Biden na Makamu wa Rais mteule Kamala Harris mbele ya Ubalozi wa Marekani Berlin, Ujerumanic Nov. 7, 2020.
8
Kiongozi wa waliowachache katika Baraza la Seneti Chuck Schumer (D-NY) akisheherekea wakati vyombo vya habari vikitangaza kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokratik Joe Biden ametajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais, Marekani, November 7, 2020, akiwa mjini Brookly New York , Marekani, Novemba 7, 2020. REUTERS/Dane Rhys