Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden, ambaye anajulikana katika duru za siasa za Washington kwa karibu nusu karne, ametajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais Marekani na anatarajiwa kuapishwa Januari 20, na kuwa rais mwenye umri mkubwa kuliko marais wote waliopita.
#VOAElections2020 : Wamarekani washeherekea ushindi wa Rais mteule Biden
Wafuasi wa chama cha Demokratik wafurahia tangazo la vyombo vya habari kwamba mgombea kiti cha rais wa chama cha Democratic Joe Biden atakuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2020. Huku wafuasi wa Donald Trump wakiandamana kupinga ushindi huo.
9
Wafuasi wa Rais wa Marekani Donald Trump wakusanyika nje ya Bunge la Jimbo huko mjini Harrisburg, Pennsylvania, U.S., November 7, 2020 wakati vyombo vya habari vikitangaza kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokratik Joe Biden ametajwa kwamba atakuwa mshindi wa urais. REUTERS/Leah Millis
10
Wafuasi wa Rais mteule Joe Biden wakisheherekea nje ya White House, Washington, DC Novemba 7, 2020.
11
Laura Nabors, 33, aliyesafiri kutoka Mississippi, akusanyika na wafuasi wenzake wa Rais wa Marekani Donald Trump nje wakati timu ya wanasheria wakifanya mkutano na waandishi wa habari baada Joe Biden kutajwa na vyombo vya habari kwamba atakuwa mshindi wa urais uchaguzi wa 2020, huko Philadelphia, Pennsylvania, Marekani. Novemba 7, 2020. REUTERS/Mark Makela
12
Wafuasi wa Rais mteule Joe Biden na Makamu wa Rais mteule Kamala Harris wakipeperusha bendera huko Las Vegas, Nov. 7, 2020.