Papa Francis aliwasili Kinshasa Jumanne Januari 31, na kutoa wito kwa Jumuia ya Kimataifa kutojihusisha ndani ya masuala ya Afrika, na kuwaachia waafrika watanzuwe matatizo yao wenyewe.
Shambulizi la bomu katika Kanisa la Kiprotestanti mjini Kasindi, Wilaya ya Beni, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lilileta maafa makubwa kwa raia waliokuwa wanahudhuria ibada.
Mkuu wa Jeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jenerali Mbangu Masita pamoja na Makamu wake Jenerali Mutu Peke wakisimamia kuwapanga wanajeshi kuzuia waasi wa M23 walioshambulia kijiji cha Karenga, DRC.
Dunia yashuhudia matukio ya kihistoria mwaka 2022 kuanzia mabadiliko ya hali ya hewa, vita vya Ukraine, ughali wa maisha hadi nja na uhamiaji.
Leo Jumapili katika eneo la Kibumba kilometa ishirini kaskakazini mwa Mji wa Goma Kivu kaskazini inaripotiwa jeshi la Congo, FARDC, limepambana vikali na waasi wa M23 na kusababisha hali kubwa ya wasiwasi katika mji wa Goma.
Ndege ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ambayo ilikuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Bukoba na ilikuwa katika safari ya kurudi Dar es salaam kupitia Mwanza. Hadi sasa watu watatu wamethibitishwa kupoteza maisha.
Ushindani umekua mkali kwenye uchaguzi wa katikati ya mhula nchini Marekani, ikiwa ni vigumu kujua nani atachukua uwongozi kwenye bunge la taifa na magavana wa baadhi ya majimbo.
Wakazi wa vijiji karibu na mji wa Rutshuru mashariki ya Congo wanakimbia mapigano makali kati ya wanajeshi wa FARDC na wapiganaji wa M23 wanaosonga mbele na kunyakua miji zaidi.
Mahujaji milioni 21, waislamu wa madhahebu ya kishia, wakiwa wamevaa nguo nyeusi wamekusanyika katika mji wa Karbala nchini Iraq kuadhimisha siku ya Arbaini, wakati nchi hiyo ikikabiliwa na misukosuko ya kisiasa.
Rais Joe Biden aliongoza ibada kwenye jengo la Pentagon, huku Makamu Rais Kamala Harris akiungana na waombolezi mjini New York na mke wa rais Jill, aliongoza ibada Pennsylvania ili kuwakumbuka watu elfu 3 walofariki kwenye maeneo hayo.
Uchaguzi Mkuu umepangwa kufanyika Angola August 24, 2022 kumchagua Rais na Wabunge President. Vuguvugu la uchaguzi linaendelea nchini humo huku kampeni zikifikia ukingoni. Rais aliyeko madarakani João Lourenço anagombea awamu yake ya pili.
Upigaji kura ukiendelea siku ya Jumanne katika uchaguzi mkuu wa urais nchini Kenya. Hali ya upigaji kura imeripotiwa kuwa shwari.
Pandisha zaidi