Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 13:20

Waliouwawa shambulizi la kigaidi Kenya wafikia 21


Inspekta Jenerali wa Kenya Joseph Boinnet

Idadi ya waliouawa katika shambulizi la kigaidi nchini Kenya imefikia 21, baada ya serikali ya Kenya kutangaza kuwa miili mingine 6 imepatikana kutoka katika kifusi kilicho kuwa katika eneo hilo.

Pia taarifa iliyotolewa inasema kuwa afisa polisi mmoja alifariki kutokana na majeraha wakati akipewa matibabu maalum.

Akizungumza na vyombo vya habari Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya Joseph Boinnet ametoa taarifa hiyo Jumatano jioni.

Amefafanua kuwa kati ya waliouwawa kuna Wakenya 16, Muingereza moja, Mmarekani mmoja na wengine wa mataifa mbalimbali.

Hata hivyo IGP ametahadharisha vyombo vya habari kujiepusha kutoa ripoti ambazo zinaweza kuhatarisha uchunguzi ambao unaendelea baada ya shambulizi hilo.

Mapema Jumatano asubuhi Rais Uhuru Kenyatta amesema alisema kuwa watu wenye silaha waliovamia eneo la biashara la hoteli na kuuwa watu 14, “wameuwawa” baada ya takriban masaa ishirini ya mapambano ambapo mamia ya raia waliokolewa.

Kikundi cha Al-Qaeda chenye mafungamano na kundi la Al-Shabaab kimedai kuhusika na shambulio hilo. Kikundi hicho kimekuwa kikilenga kuishambulia Kenya tangu ilipopeleka jeshi lake nchini Somalia Octoba 2011 kupambana na kikundi hicho cha wanajihadi.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Fred Matiangi, mtu mmoja alijiripua kwa kujitoa muhanga na watu wenye silaha walipambana na majeshi katika kurushiana risasi wakati wa shambulizi hilo katika eneo la DusitD2, ambalo lina vyumba vya hoteli 101, mgahawa na majengo ya ofisi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG