Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 14:53

Waliouwawa katika shambulizi la Somalia wafikia 30


Nyumba zilizoharibiwa na mlipuka wa shambulizi la mabomu mjini Mogadishu, Somalia, Jumamosi , Disemba 22, 2018.
Nyumba zilizoharibiwa na mlipuka wa shambulizi la mabomu mjini Mogadishu, Somalia, Jumamosi , Disemba 22, 2018.

Idadi ya waliouwawa na shambulizi ya magari mawili yaliokuwa na mabomu karibu na eneo la makazi ya rais Somalia imeongezeka kufikia 30 Jumapili, Polisi wamesema.

Polisi siku ya Jumamosi wameeleza kuwa watu saba waliuwawa baada ya milipuko hiyo miwili mjini Mogadishu, ambayo kundi la wanajihadi wa Al-Shabaab walidai kuhisika na shambulizi hilo.

“Idadi ya walio waliouwawa katika milipuko hiyo imeongezeka na kufikia watu 20 na zaidi ya watu 40 wamejeruhiwa,” amesema afisa mmoja wa polisi, Ibrahim Mohamed.

Amesema idadi ya vifo imeongezeka baada ya baadhi ya wale waliojeruhiwa kufa wakiwa hospitali.

Pande zote raia na vikosi vya usalama ni kati ya wale walioathirika na shambuliz hilo, maafisa wamesema.

Kituo cha Televisheni cha Somalia kinacho endesha shughuli zake Uingereza kimesema kuwa watatu kati ya wafanyakazi wake ni miongoni wa waliouwawa, wakimtaja mmoja wao Awil Dahir kuwa aliokuwa na uraia pacha wa Somalia na Uingereza.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed amelaani “mashambulizi yasiyo kuwa na ushujaa”.

“Tutaendelea kuwashinda magaidi ili tuweze kuongoza wananchi wa Somalia kwenda kwenye utulivu na mafanikio,” amesema katika tamko lake.

Waziri Mkuu wa Somalia Hassan Ali Khaire aliwatembelea wale wote waliojeruhiwa.

XS
SM
MD
LG