Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 01:19

Rais Farmajo wa Somalia anusurika kuondolewa madarakani


Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo

Wabunge wa upinzani na wale wanaomuunga mkono Rais Farmajo walikubaliana Alhamis kwa maandishi kwamba hoja ya kumfungulia mashtaka ilikuwa sio sahihi

Wiki kadhaa za majibizano na mazungumzo katika bunge la Somalia zimesitisha juhudi za kumuondoa madarakani Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo kwa kumshtaki kumuondoa mamlakani.

Wabunge wa upinzani pamoja na wale wanaomuunga mkono Rais Farmajo walikubaliana Alhamis kwa maandishi kwamba hoja ya kumfungulia mashtaka ilikuwa sio sahihi. Farmajo alishutumiwa kukiuka katiba kwa kutia saini kile wapinzani wake walichosema ilikuwa mikataba ya siri ya biashara na Ethiopia na Eritrea pamoja na kufanya maamuzi ya peke yake ya kuteuwa majaji na makamanda wa jeshi.

Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo
Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo

​Hoja ya kumfungulia mashtaka rais inahitaji uungaji mkono wa wabunge 92 kati ya 275. Wabunge 14 ambao waliorodheshwa kwenye hati walilalamika kwamba hawakutia saini karatasi yeyote.

Uongozi wa bunge pia ulidai kwamba juhudi za kumfungulia mashtaka zilipelekwa katika mahakama isiyo sahihi. Hoja kama hiyo ilitokea mwezi Machi dhidi ya spika wa zamani wa bunge la Somalia Profesa Mohamed Osman Jawari na ilisababisha mzozo mkali juu ya uhalali wa hatua hiyo na hatimaye Jawari aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG