Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 12:06

Rais wa Somalia Farmajo yupo Eritrea kwa siku 3


Rais wa Somalia Farmajo akiwa na Rais wa Eritrea Afwerki mjini Asmara
Rais wa Somalia Farmajo akiwa na Rais wa Eritrea Afwerki mjini Asmara

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo siku ya Jumamosi alianza ziara ya siku tatu ya kihistoria kwenda Eritrea, mahala ambako amefanya mazungumzo na kiongozi mwenzake mjini Asmara. Waziri wa habari wa Eritrea alitangaza Ijumaa kwamba kiongozi huyo wa Somalia alialikwa na Rais wa Eritrea, Isaias Afwerki.

Msemaji wa rais wa Somalia, Abdinur Mohamed aliandika Jumamosi kwenye Twitter “Somalia ipo tayari kuandika ukurasa mpya wa uhusiano wake na Eritrea”. Nchi hizi mbili hazijawahi kuwa na ushirikiano wowote wa kidiplomasia kwa takribani miaka 15 lakini msemaji wa rais wa Somalia, alisema ziara hiyo itafungua milango kwa uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano mpya kati ya mataifa hayo mawili.

Bendera za Somalia na Eritrea zilipepea pembeni ya mitaa ya mji mkuu wa Eritrea, Asmara kabla ya ziara hiyo kuanza. Ziara ya Farmajo imekuja baada ya mahasimu wa muda mrefu nchi ya Eritrea na Ethiopia kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia hatua ambayo ilimaliza kutengwa kwa Eritrea kieneo na kimataifa kulikodumu kwa takribani miongo miwili.

XS
SM
MD
LG