Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 06:21

Al-Shabaab yasema imehusika na mauaji ya wanajeshi 7 Somalia


Wapiganaji wa al-Shabaab wakiwa katika mazoezi yao ya kivita, wakiongozwa na mtoto mdogo katika kitongoji cha Suqaholaha, karibu na Mogadishu, Somalia, Januari. 1, 2010.

Serikali ya Somalia imeeleza kuwa wanajeshi wake 7 wameuwawa Alhamisi katika mji mdogo wa Wanalaweyn, kusini magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu, katika shambulizi la bomu.

Kundi la al-Shabaab limesema kuwa lilihusika na mashambulizi hayo mawili, yaliyotokea siku ya Jumatano na Alhamisi.

Naibu Gavana wa Jimbo la Shabelle Ali Nur ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanajeshi hao waliuwawa pamoja na kamanda wao wakati bomu lilipolipua gari waliokuwa wakisafiria wanajeshi hao.

Shambulio hilo ni la pili kufanyika katika muda wa siku mbili baada ya shambulio jengine kutokea Jumatano katika mji huo wa wanalaweyn na kuwaua watu 14.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG