Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 23:35

Mapambano Somalia yameuwa takribani watu 13


Mapambano kati ya wanajeshi wa Somalia wanaowaunga mkono wanavijiji na wanamgambo wa kundi la al-Shabaab yamesababisha vifo vya takriban wapiganaji 13, walioshuhudia na maafisa walisema.

Mapambano huko kati kati ya Somalia yaliyotokea Jumamosi yalianza baada ya wanamgambo waliokuwa na silaha wa kundi la Al- Shabaab walipojaribu kuweka kodi kwa wakazi wa Halfoley, kijiji kimoja kilicho karibu na mji wa Jalalagsi katika wilaya ya Hiran.

Mkuu wa wilaya katika mji wa Bulabarde, Abdi Dahir Guure aliaambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba wanajeshi wa serikali wanaowasaidia wafugaji walishiriki katika mapambano makali ya zaidi ya saa tano za ufyatuaji risasi na wanamgambo.

Maafisa wa serikali ya Somalia katika wilaya walisema vitengo vingine vya jeshi la taifa la Somalia viliingia katika vijiji vingine kwenye wilaya hiyo kuwazuia wanamgambo kujipanga tena na kufanya tena mashambulizi yanayosababisha vifo na uharibifu.

XS
SM
MD
LG