Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 01:08

Walebnani wasema haijatosha kujiuzulu Hariri


Waziri Mkuu Saad Al-Hariri
Waziri Mkuu Saad Al-Hariri

Kwa mara nyingine tena maandamano ya wananchi yafanikiwa kuuondoa utawala wa nchi ya kiarabu madarakani.

Safari hii baada ya maandamano ya siku 12 wananchi wa Lebanon wamemlazimisha Waziri Mkuu Saad Al-Hariri kujiuzulu pamoja na serikali yake.
Licha ya mabadiliko hayo waandamanaji wamesema wataendelea na malalamiko yao hadi madai yote yanatekelezwa.

Hali ilivyokuwa Lebanon

Maelfu ya Walebnani kutoka kila pembe ya nchi walishuka katika viwanja vikuu vya miji yao usiku kusherehekea ushindi wao wa Jumanne pamoja na kulaani ghasia zilizozuka Beirut muda mfupi kabla ya Waziri Mkuu Msuni Saad Hariri kutanagaza anajiuzulu.

Ghasia hizo zilisababishwa na wafuasi wa kundi la kishia la Hezbollah linaloongozwa na Imam Hassan Nasrallah na kundi la Amal la Nabih Berri. Wapinzani hao walijaribu kuvunja kambi ya waandamanaji nje ya jengo kuu la serikali na kutia moto baadhi ya mahema yaliokuwepo.

Licha ya ghasia hizo waandamanaji walijitokeza usiku wa Jumanne na kusema wataendelea hadi kupata ushindi kamili. Abdallah Hammoud muandamanaji mjini Beirut akizungumza na shirika la habari la Reuters, amewapongeza waandamanaji kwa ushindi wao.

Hammoud anaelezea kuwa wananchi wamepata ushindi dhidi ya mabwanyenye wa kisiasa katika nchi hii. "Tutaendelea na vuguvugu letu, na uasi wetu, katika mapinduzi yetu ya kuwaondoa wezi wa mali waliolitumbukiza taifa hili katika janga la kiuchumi.

Waziri Mkuu tajiri Hariri akilihutubia taifa hapo Jumanne alisema kwa huzuni kwamba uamuzi wake unatokana na dhamira ya Walebanon wengi walioshuka mitaani wakitaka mabadiliko katika kile alichokieleza maandamano ya kihistoria.

Kilio cha wananchi

Waziri Mkuu wa lebanon amesema : Nimejaribu mnamo kipindi hichi kusikiliza kilio cha wananchi na kulilinda taifa kutokana na hatari za kiuchumi, kijamii na usalama. Lakini leo hii ninasema nimegonga mwamaba."

Wananchi waliokuwa wakisikiliza hotuba hiyo walisherehekea alipotangaza anajiuzulu ikiwa ni mara yake ya tatu kuacha nafasi hiyo.

Kujiuzulu kwa Hariri ni kukaidi wito wa mshirika wake Hezbollah katika serikali ambaye kiongozi wake Nassarallah alionya kwamba nchi itatumbukia katika ghasia.

Wiki iliyopita Hariri alifanya mabadiliko makubwa ya baraza lake la mawaziri na kupendekeza mageuzi ya kiuchumi mambo ambayo hayajawaridhisha waandamanaji wanaotaka kuwaona wanasiasa wote wanaodai ni walaji rushwa wameondolewa na kufanyika mageuzi kamili ya utawala kugawanya madaraka kwa misingi ya kidini.

Waandamanaji kwa ujumla wameridhika na uwamuzi wa Hariri kujiuzulu lakini wanataka viongozi wengine wote waondoke kama anavyoeleza Aya al Amari mwanafunzi wa miaka 19.

Aya al-Amari, Mwanafunzi

Tunashukuru saad Hariri amejibu matakwa ya wananchi na tuna matumaini wengine watasikiliza maombi ye wananchi na kujiuzulu vile vile. Hicho ndicho tunachotaka. Hatutaki ulaji rushwa, na atuwataki. Tunataka taifa ambalo tunaliamini.

Ufaransa mshirika mkubwa wa Hariri na mtawala wa kikoloni wa taifa hiolo ametowa msaada wa dola bilioni 11 kwa ajili ya maendeleo nakuepusha nchi kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwishoni mwa miaka 1990.

Kulingana na katiba Baraza la mawaziri linaendelea na kazi hadi pale wabunge wanafikia makubaliano ya kumchagua waziri mkuu mpya.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG