Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 10:47

Trump asema Iran haisikii na itaendelea 'kumulikwa'


Jaribio la kombora la masafa marefu lililofanywa na Iran
Jaribio la kombora la masafa marefu lililofanywa na Iran

Marekani imechukua hatua za kwanza kuendeleza msimamo mkali kuhusu Iran, ikiweka vikwazo vipya kwa watu binafsi 13 na makundi 12 wanaoshirikiana nao katika programu ya kombora la masafa marefu.

Wale ambao wanahusishwa na programu ya kombora la masafa marefu na washirika wao ni pamoja na China, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Lebanon.

Rais Donald Trump amesema kuwa Iran imekuwa haisikii na itaendelea kumulikwa. White House inaamini kuwa itachukuwa hatua za kuishinikiza Iran katika jaribio lake la kombora la masafa marefu, wakati Rais Trump akionya kuwa: Iran haitaki kusikia.

Pia vikwazo hivyo vimelenga mitandao inayoisaidia Iran huko China na Umoja wa Falme za Kiarabu ambazo zimekuwa zikiwasaidia Tehran kufikia teknolojia kwa kuwauzia malighafi inayohitajika katika mradi huo.

Wizara ya Fedha pia imesema vikwazo vimewekwa pia kwa watu na mitandao inayofanya kazi na kikos maalum cha ulinzi cha Iran (Islamic Revolutionary Guard Corps’ elite Quds Force) na kundi la kigaidi la Lebanon la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran.

“Hizi ni hatua za mwanzo katika kukabiliana na tabia ya uchokozi ya Iran,” afisa wa ngazi ya juu wa utawala wa Trump ameonya, akiongeza kuwa tabia ya Iran hivi karibuni “haivumiliki na haikubaliki.”

Iran inahiari kuchagua

“Iran ina hiyari ya kuchagua,” afisa huyo amesema. “Sisi tutakuwa tayari kufanya kazi na Iran pale tu itapotekeleza ahadi zake za kimataifa na tunasisitiza dhamira yetu iko pale pale katika kutumia nguvu kuzuia vitendo vya uharibirifu vya Iran.”

Wizara ya Fedha ya Marekani imetangaza vikwazo vipya kwa Iran ikijibu kitendo chake cha kufanya jaribio la kombora hivi karibuni.

Tangazo hilo linafuatia onyo lililotolewa Ijumaa na rais wa Marekani Donald Trump kwa Iran baada ya waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo kutupilia mbali vitisho vya Marekani kufuatia jaribio la kombora.

“Iran inacheza na moto—hawana shukrani juu ya “ukarimu” aliowafanyia Rais Barack Obama. Lakini sio mimi!,” Trump alituma ujumbe wa Twitter.

Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alituma ujumbe wa Twitter Ijumaa, akisema Iran haitotetereka kwa vitisho vya Marekani. “Iran haitoyumbishwa na vitisho kwani sisi tunapata usalama wetu kutoka kwa wananchi,” Zarif ameandika.

Mshauri wa Usalama wa Taifa Michael Flynn ameweka wazi katika tamko lake Jumamosi : “Siku za kufumbia macho uchokozi wa Iran na vitendo vyake vya uadui dhidi ya Marekani na jumuiya ya kimataifa zimefikia ukingoni,”

Usalama wa Taifa

Kabla ya rais kuondoka White House kuelekea Mar-a-Lago huko Florida Ijumaa, alikula chakula cha mchana na Mshauri wa Usalama wa Taifa Michael Flynn. Flynn pia alifanya mazungumzo ya simu na mwanadiplomasia wa juu wa China, Yang Jiechi.

Katika taarifa yake baada ya mazungumzo hayo, waziri wa mambo ya nje alimwambia Flynn China inatarajia kufanya kazi pamoja na Marekani katika hatua za kutatua migogoro na kuwa nchi hizo mbili zinamaslahi ya pamoja.

XS
SM
MD
LG