Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 12:47

Kuwait yaikabidhi Qatar masharti mapya kabla ya kuondolewa vikwazo


Wafanyakazi wa kituo cha Al-Jazeera. Kituo hiki kimetakiwa kufungwa na baadhi wa mahasimu wa Qatar walioiwekea vikwazo.
Wafanyakazi wa kituo cha Al-Jazeera. Kituo hiki kimetakiwa kufungwa na baadhi wa mahasimu wa Qatar walioiwekea vikwazo.

Saudi Arabia pamoja na mataifa mengine ya ghuba yaliovunja uhusiano na Qatar kutokana na madai ya kufadhili ugaidi yametoa ordha ya mambo yanayohitajika kutekelezwa na Qatar.

Kuwait ambayo ni mpatanishi wa Qatar na mataifa ya Saudi Arabia, Bahrain, Umoja wa falme za kiarabu pamoja na Misri imewasilisha masharti hayo kwa Qatar.

Katika masharti hayo wameitaka Qatar kuvunja uhusiano na nchi ya Iran, kufunga ubalozi wake nchini humo, na pia kufunga kituo cha habari cha Al Jazeera pamoja na vituo shirika.

Taarifa hiyo imesema kuwa masharti mengine ni pamoja na kuvunja uhusiano wowote ule na makundi ya kigaidi yakiwemo ya kikundi cha Muslim Brothehood, Iskamic State, al Qaida pamoja na lile la Hezbollah kutoka Lebanon.

Nchi hizo ambazo zimeiwekea vikwazo Qatar zimeitaka Qatar iondoshe wanajeshi wa Uturuki walioko nchini humo pamoja na kusitisha ushirikiano wa kijeshi na Uturuki.

XS
SM
MD
LG