Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 03:23

Trump atuma ujumbe wa Tweet kukanusha madai juu ya Comey


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump wa Marekani amesema Alhamisi hakuwa amerikodi mazungumzo yake na aliyekuwa mkuu wa FBI James Comey.

Comey amesema rais alimhimiza kusitisha uchunguzi uliokuwa unafanywa na FBI dhidi ya Russia katika kile kinachosadikiwa kuwa iliingilia kati uchaguzi wa rais mwaka 2016, jambo ambalo Trump anakanusha.

Trump aliandika katika akaunti yake ya Twitter: “Pamoja na ripoti zote za hivi karibuni katika uchunguzi wa kieletronikia, kuingilia mitandao ya mawasiliano, na kufichua na uvujishaji wa habari kinyume cha sheria, mimi sina habari kuwa kulikuwa na rekodi zilizosajiliwa kwenye kinasa sauti kuhusu mazungumzo yangu na James Comey, lakini Mimi sikufanya hivyo, na sina rekodi au mfano wa hicho.”

Ujumbe wa tweet ulimaliza wiki ya mashaka iwapo rais alikuwa ametegesha vinasa sauti katika ikulu ya White House na kurekodi mazungumzo kati yao mara mbili.

“Sijui kama huo ni mchezo,” Naibu Msemaji wa White House Sarah Huckabee Sanders amesema alipoulizwa kwa nini rais alisubiri kwa siku 41 kabla ya kutoa ufafanuzi kuwa hakuna kinasa Sauti kilichotumika kurikodi mazungumzo yake na Comey.

“Watu nyie mlikuwa mnauliza jawabu, nimewapeni,” aliongeza kusema Sanders wakati akihojiwa bila ya kamera kwenye muhtasari wake kwa vyombo vya habari baada ya rais kutuma ujumbe kuhusu suala hilo.

XS
SM
MD
LG