Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 08:18

Islamic State yadai kutekeleza shambulizi la Uturuki


Jamaa wa Fatih Cakmak muathirika wa shambulizi la Reina wakiwa katika mazishi yake mjini Istanbul.
Jamaa wa Fatih Cakmak muathirika wa shambulizi la Reina wakiwa katika mazishi yake mjini Istanbul.

Kati ya watu 39 waliouwawa 25 ni raia wa kigeni, wakiwemo kutoka Jordan, Lebanon, Israel, Saudi Arabia, Iraq na Canada

Kundi la Islamic State limedai Jumatatu kuhusika na shambulizi la mwaka mpya katika klabu ya usiku huko Istanbul, Uturuki ambapo watu 39 waliuwawa na tayari vyombo vya usalama vinaendelea kumsaka muuwaji aliyetoweka baada ya shambulizi.

Kundi hilo limesema katika taarifa yake “ askari wa khalifa” ndiye alifanya shambulizi hilo.

Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti Jumatatu kwamba tayari watu wanane wametiwa nguvuni kutokana na shambulio hilo lakini aliyefanya mauaji siyo kati yao.

Shambulizi hilo lilianza mapema Jumapili wakati mtu mwenye silaha alipomuua afisa polisi na raia nje ya klabu ya usiku ijulikanayo kama Reina kabla ya kuingia ndani. Kulikuwa na takriban watu 600 kwenye klabu hiyo wakati huo, ambapo baadhi walikimbilia katika eneo la Bosporus ili kujinusuru.

Vyombo vya usalama vimesema muuaji huyo kwanza alijichanganya na watu waliokuwa wakiondoka hapo klabu. Pamoja na wale waliouwawa kulikuwa na watu 70 waliojeruhiwa.

Viongozi walaani shambulizi la Uturuki

Rais Recep Tayyip Erdogan ameliita shambulizi hili ni “shambulizi la kinyama” katika taarifa yake Jumapili.

“Uturuki itashikamana na haitatoa njia ya michezo michafu ya magaidi,” alisema.

Viongozi kote ulimwenguni wamelaani vikali shambulizi hilo.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema amelaani vikali “shambulizi la kigaidi” na anatarajia wale wote waliohusika kuliandaa na kulitekeleza watafikishwa haraka katika vyombo vya sheria .

Viongozi waahidi kuisaidia Uturuki kupambana na ugaidi

Katika ujumbe wake kwa Erdogan, Rais wa Russia, Vladimir Putin ameahidi kuisaidia Uturuki katika kupambana na ugaidi, kwa mujibu wa tamko la Kremlin.

“Ni vigumu kufikiria tukio kubwa la uhalifu wa kinyama zaidi ya mauaji ya watu wasio na hatia katika sherehe za mwaka mpya,” alisema Putin.

XS
SM
MD
LG