Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 13:05

Wajerumani wapiga kura kumchagua kiongozi mpya


Mtu akipiga kura yake wakati wa uchaguzi Mkuu, Berlin, Ujerumani, Septemba 26, 2021. REUTERS/Fabrizio Bensch
Mtu akipiga kura yake wakati wa uchaguzi Mkuu, Berlin, Ujerumani, Septemba 26, 2021. REUTERS/Fabrizio Bensch

Wajerumani milioni 60 wanaostahiki kupiga kura wataiweka nchi yao katika mwelekeo mpya katika uchaguzi wa bunge unaofanyika Jumapili.

Wabunge watakao shinda uchaguzi wataamua nani atakayemrithi chansela wa nchi hiyo maarufu anayeachia madaraka, Angela Merkel.

Wanasiasa watakao chaguliwa upya kuna uwezekano watalazimika kuunda serikali ya mseto, ikimaanisha kuwa huenda ikachukua wiki kadhaa kabla ya mrithi wa Merkel kutangazwa.

Merkel, ambaye ndiye chachu ya Ujerumani kufikia nafasi ya kuwa uchumi unaongoza Ulaya, anaachia madaraka baada ya kuongoza kwa miaka 16 katika wadhifa wa juu, kwenye serikali iliyoongozwa na chama cha mrengo wa kati cha Christian Democratic Union.

Merkel amekuwa anasita kuonyesha kumuunga mkono kiongozi yeyote wa vyama mbalimbali wanaoiwania nafasi yake, akiwemo makamu chansela wake, Olaf Scholz wa chama cha Social Democratic.

Hata hivyo, Siku ya Jumamosi, kiongozi huyo wa Ujerumani alihudhuria kampeni ya Armin Laschet, kiongozi wa chama cha Christian Democrats.

XS
SM
MD
LG