Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 03, 2023 Local time: 02:54

Mlipuko wa bomu Mogadishu waua watu wasiopungua saba


Mlipuko wa bomu katika mji wa Mogadishu
Mlipuko wa bomu katika mji wa Mogadishu

Bomu la kwenye gari la kujitoa muhanga limewaua watu wasiopungua saba katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Mlipuko huo umetokea Jumamosi kwenye makutano ya barabara karibu na makazi ya rais, afisa mmoja amesema.

Muawiye Mudeey, mkuu wa wilaya ya Hamarjajab ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba mlipuko huo ulitokea kwenye makutano yaliyo mjini Ceelgaab.

Haikufahamika mara moja ni nani aliyehusika na shambulio hilo, lakini al-Shabaab, kundi la wanamgambo ambalo lina azma ya kuiondoa madarakani serikali na kusimika sheria za Kiislamu, mara nyingi limehusika na ulipuaji mabomu kama hayo.

Shahidi mmoja katika eneo la tukio ameiambia Reuters kwamba, ameona magari saba na tuktuk tatu, zikiwa zimeharibiwa na mlipuko huo, huku eneo palipotokea mlipuko huo likiwa limejaa damu.

Chanzo cha habari hii ni REUTERS/AFP/AP

XS
SM
MD
LG