Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 09:56

Kamati maalum kuchunguza kutoweka kwa jasusi, kubuniwa Somalia


Rais wa Somalia Abdullahi Farmajo kwenye picha ya maktaba
Rais wa Somalia Abdullahi Farmajo kwenye picha ya maktaba

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo ametangaza kuunda kamati maalum ya kuchunguza kesi ya jasusi aliyetoweka na ambaye alitangazwa kufa na idara ya taifa ya ujasusi nchini humo,  NISA, ingawa bado haijafahamika muda aliotoweka wala alipo.  

Idara ya NISA mapema mwezi huu ilisema kwamba Bi Ikran Tahlil Farah alitoweka Juni na kwamba alitekwa nyara na kuuwawa na wanamgambo wa al- Shabab. Hata hivyo al- Shabab wamekanusha madai hayo wakati mama wa jasusi huyo Qali Mohamud Guhad akiilaumu NISA kutokana na kifo kinachodaiwa kutokea.

Guhad ameikataa kamati ya uchunguzi ya rais ambayo itajumuisha mwakakilishi kutoka NISA. Guhad wakati akiongea na VOA Idhaa ya kisomali alisema kwamba kiongozi wa nchi hajasema lolote kwa zaidi ya miezi mitatu tangu kutoweka kwa mwanawe.

Ameongeza kusema kwamba ana imani na mahakama ya kijeshi inayoendelea kufanya uchunguzi kuhusu kutoweka kwa Farah. Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Abdimalik Abdullahi amesema kwamba ni jeshi pekee linaloweza kufanya uchunguzi wa kina kwa kuwa taasisi nyingine za serikali haziaminiki.

XS
SM
MD
LG