Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:34

Raiya wawili wa kigena wafungwa jela Somalia


Raiya wa Somalia wasaidia mtu aliyejeruhiwa kwenye shambulizi la kigaidi mjini Mogadishu
Raiya wa Somalia wasaidia mtu aliyejeruhiwa kwenye shambulizi la kigaidi mjini Mogadishu

Mahakama ya kijeshi nchini Somalia Alhamisi imewahukumu raia wawili wa kigeni wenye itikadi kali kwa kupigana wakiwa upande wa kundi la kigaidi la Al Shabab.

Mahakama hiyo mjini Mogadishu imewahukumu Darren Anthony Byrnes kutoka Uingereza na Ahmad Mustakin Bin Abdul Hamid kutoka Malaysia kifungo cha miaka 15 jela, kwa kuwa wanachama wa al Shabab na kuingia Somalia kinyume cha sheria.

Ni raia wa kwanza wa kigeni wenye itikadi kali kuhukumiwa nchini Somalia kwa sababu ya uanachama wao kwa Al Shabab, maafisa wa mahakama wamesema.

Waendesha mashtaka wamesema Abdul Hamid na Byrnes waliingia Somalia ili kuunga mkono Al Shabab na ‘kuharibu’ na ‘kumwaga damu’.

Wakili wao, Mohamed Warsame Mohamed amesema wanaume hao walikanusha uanachama wao katika kundi la Al Shabab na kudai kwamba walikuja Somalia kutembelea jamaa na marafiki.

Mohamed amesema, hakuna mashahidi wanaounga mkono utetezi wa serikali mahakamani. Anasema badala yake, serikali imetumia maelezo ya watu waliotoa ushahidi bila kuwepo mahakamani na madai kwamba washtakiwa walikiri kuwa wanachama wa Al Shabab.

XS
SM
MD
LG