Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:09

Mwanamke wa kwanza kuwania urais ,Somalia


Wabunge wa Somali kwenye picha ya awali
Wabunge wa Somali kwenye picha ya awali

Mwanamke wa kwanza nchini Somalia ambaye amevunja vikwazo  na kuwa waziri wa mambo ya nje pamoja na naibu waziri mkuu sasa analenga kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ambao umecheleweshwa kwa muda mrefu. 

FawziaYusufu H.Adam anafahamu vyema changamoto zinazomkabili kupata uungaji mkono kwenye taifa ambalo mara nyingi linawabagua wanawake. Ingawa wanawake wengi wamesoma kwenye mataifa ya kigeni, na sasa wanarejea Somalia ili kuchangia kwenye ujenzi wa taifa baada ya mapigano ya miongo mitatu, kukubalika kwa mwanamke kama rais bado ni changamoto.

Wakati akifanya mahojiano na shirika la habari la AP,Fawzia alisema kwamba hata kuongoza wafanyakazi kwenye wizara ya mambo ya nje ambapo wafanyakazi wengi ni wanaume ni changamoto , akiongeza kuwa baadhi wanakataa kutoa ushirikiano kwake kutokana na kuwa yeye ni mwanamke.

Amesema kwamba hata baadhi ya marafiki zake hawaamini kwamba anaweza kuongoza taifa hilo kutokana na jinsia yake. Abdiwahid Mohamed Adam ambaye ni daktari kwenye hospitali moja mjini Mogadishu amesema kwamba Fauzia ni kiongozi mzuri lakini kwa bahati mbaya ni mwanamke ambaye hawezi kukubalika kwa urahisi nchini Somalia.

XS
SM
MD
LG