Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 10:02

Kagame : Jeshi la Rwanda litaendelea kulinda usalama Msumbiji


Wanajeshi wa Msumbiji wakikaguliwa na Rais wa Mozambique Filipe Nyusi na Rais wa Rwanda Paul Kagame Sept. 24, 2021, Pemba, Mkoa wa Cabo Delgado, Mozambique.
Wanajeshi wa Msumbiji wakikaguliwa na Rais wa Mozambique Filipe Nyusi na Rais wa Rwanda Paul Kagame Sept. 24, 2021, Pemba, Mkoa wa Cabo Delgado, Mozambique.

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema vikosi vya serikali yake vitasaidia kuhakikisha hali ya usalama na kujenga tena maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji, yaliyoharibiwa na waasi wa Kiislamu.

Kagame alisema hayo Ijumaa wakati maafisa wa serikali ya Msumbiji wakianza kuhamasisha raia wa nchi hiyo kurudi makwao katika eneo hilo lenye utajiri wa gesi.

Umoja wa Mataifa umeonya juu ya tishio linaloendelea la wanamgambo huko Cabo Delgado, ambako vikosi vya Rwanda vinashika doria katika barabara zilizotelekezwa na waasi ambao kwa wakati mmoja walikuwa wanazingira.

Kagame aliuambia mkutano wa waandishi wa habari katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo, akiwa pamoja na mwenzake wa Msumbiji Filipe Nyusi kwamba "Ujumbe wa wanajeshi wa Rwanda nchini Msumbiji unaendelea."

Alisema mikakati mipya inapaswa kuwepo kuhakikisha usalama katika maeneo yaliyokombolewa hadi ujenzi utakapomalizika.

Kagame alisema wanajeshi wake watakaa kwa muda mrefu zaidi kama Msumbiji itawahitaji kufanya hivyo.

Wanajeshi wa Rwanda na Msumbiji wanadhibiti baadhi ya sehemu za kaskazini mwa Cabo Delgado - eneo linalokadiriwa kuwa na miradi ya gesi yenye thamani ya dola bilioni 60 limekuwa likishambuliwa na wanamgambo hao tangu mwaka 2017.

Chanzo cha habari hii ni REUTERS/AFP/AP

XS
SM
MD
LG