Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:11

Wanajeshi wakabiliana na waasi Cabo Delgado , Msumbiji


Fishermen cast their nets beneath the skyline of Mozambique's capital Maputo in this file picture taken Nov. 2009.
Fishermen cast their nets beneath the skyline of Mozambique's capital Maputo in this file picture taken Nov. 2009.

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi Jumapili amesema wanajeshi wanaopambana na waasi wenye uhusiano na kundi la Islamic State katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado wanaendelea kupata ushindi uwanjani na adui amerudi nyuma.

Nyusi alikuwa akilihutubia taifa kuhusu mzozo uliopamba moto wakati waasi wakishambulia mji wa pwani wa Palma mwezi March, karibu na miradi ya gesi yenye thamani ya dola billioni 60 ambayo ilikua inalenga kubadilisha uchumi wa Msumbiji.

Akitoa hotuba hiyo kupitia televisheni na mitandao ya kijamii, Nyusi ametangaza kwamba wanajeshi wa SADC wanahamasishwa kuingilia kijeshi katika mkoa wa Cabo Delgado, ulioko chini ya uasi wa kijihadi.

Ombi la SADC kuingilia kati huko Cabo Delgado limekamilishwa rasmi, waziri wa ulinzi wa Msumbiji, Jaime Neto ameliambia shirika la habari la AFP, kwa njia ya simu.

XS
SM
MD
LG