Kikundi cha Waislam hao kilishambulia makanisa na makazi ya Wakristo walio wachache, na kusababisha mamlaka husika kuwataka wanajeshi kutuliza ghasia, maafisa walisema Alhamisi.
Hakuna majeruhi wakati Wakristo wanaoishi katika eneo hilo la makazi katika mji wa Jaranwala kwenye wilaya ya Faisalabad kuondoka haraka kuelekea maeneo salama pamoja na familia zao kufuatia moja ya mashambulizi mabaya kabisa kutokea nchini humo dhidi ya Wakristo.
Wakristo walianza kurejea pole pole majumbani mwao Alhamisi, na kujionea uharibifu kwenye kanisa moja lililochomwa moto. Makanisa mengine manne pia yaliharibiwa. Nyumba dazeni mbili zilikuwa zimechomwa moto au kuharibiwa vibaya sana wakati wa ghasia hizo.
“Tulikuwa nyumbani tumepumzika wakati ghafla tulisikia kikundi kimoja kinakuja na kuchoma nyumba na kuvamia makanisa,” Shazia Amjad alisema, huku akilia nje ya nyumba yake, ambayo ilichomwa moto Jumatano.
Mwanamke huyo Aliliambia shirika la habari la Associated Press kuwa wale walioanya ghasia walichoma moto vitu vya nyumbani na samani. Baadhi ya vitu vya Amjad viliibiwa wakati alipoondoka yeye na familia yake kukimbilia sehemu salama, aliongeza kusema.
Amjad alieleza kuwa waliofanya ghasia walimwaga mafuta ya petrol ili kuchoma nyumba katika maeneo yao, na waliiba pia vitona vitu vingine. Wakristo wengine walieleza madhila skama hayo na kuonyesha mshangao mkubwa.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.
Forum