Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 09, 2024 Local time: 02:54

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Khan, ahukumiwa kifungo cha miaka 3 gerezani


Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan

Polisi wa Pakistani Jumamosi walimkamata Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan, dakika chache baada ya mahakama ya serikali kuu kumhukumu kifungo cha miaka mitatu gerezani, kwa tuhuma za kuuza zawadi za serikali kinyume cha sheria.

Mwanasiasa huyo maarufu mwenye umri wa miaka 70 aliwekwa chini ya ulinzi katika mji wa mashariki wa Lahore, na alikuwa akipelekwa katika gereza moja katika mji mkuu wa taifa, Islamabad, ambapo hukumu hiyo ilitangazwa, wawakilishi wa serikali na Khan walisema.

Isipokuwa ibatilishwe na mahakama ya rufaa, hukumu hiyo itamuondoa Khan katika siasa za kitaifa kwa miaka mitano na kuondoa uwezo wake wa kugombea uchaguzi ujao wa Pakistani, uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu, walisema wataalam wa sheria, wakinukuu sheria za uchaguzi. Chama cha kisiasa cha Khan, Pakistan Tehreek-e-Insaf, kilisema kimewasilisha rufaa ya uamuzi huo kwa haraka, katika Mahakama ya Juu.

"Ni jambo la aibu na la kuchukiza sana jinsi dhihaka za sheria zinavyoendelea kwa sababu tu nia ni kumzuia kisiasa na kumfunga Imran Khan jela," PTI ilisema katika taarifa yake.

Hukumu hiyo inahusiana na uchunguzi wa tume ya uchaguzi nchini humo, ambayo ilimpata kiongozi huyo wa zamani, ambaye paia alikuwa mchezaji maarufu wa kriketi, na hatia ya kuuza zawadi za serikali kinyume cha sheria akiwa waziri mkuu kuanzia 2018 hadi 2022.

Forum

XS
SM
MD
LG