Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:01

Mlipuko waua zaidi ya watu 40 nchini Pakistan


Wafanyakazi wa ukoaji wakimbeba mtu aliyejeruhiwa baada ya mlipuko katika wilaya ya Bajur, jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, Julai 30, 2023.

Mlipuko katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Pakistan la Khyber Pakhtunkwa uliua zaidi ya watu 40, maafisa wamesema.

.Mlipuko huo ulitokea katika mji wa Khar unaokaliwa na kabila la Wabajaur, ambao uko karibu na mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan. Ulitokea Jumapili alasiri wakati wa mkutano wa wafanyakazi wa chama cha kidini, Jamiat Ulema Islam (JUI).

Akizungumza kwa njia ya simu na VOA, afisa wa afya wa wilaya Dr Faisal Kamal alithibitisha vifo 43 na kutoa idadi ya watu 80 waliojeruhiwa. Awali, vyanzo vingine vilitoa idadi ya watu 150 waliojeruhiwa.

Afisa wa polisi wa wilaya Nazeer Khan ameiambia VOA kwamba ushahidi uliokusanywa kufikia sasa unaonyesha kuwa mlipuko huo ni kitendo cha mshambuliaji wa kujitoa mhanga.

Katika ujumbe kwenye Twitter, waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan Rana Sanaullah alisema uchunguzi kuhusu tukio hilo uliamriwa.

Forum

XS
SM
MD
LG