Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 10:37

Pakistan yapitisha bajeti kukidhi masharti ya IMF


Bunge la Pakistan, Jumapili limeidhinisha bajeti ya serikali ya mwaka 2023 - 2024 ambayo ilirekebishwa ili kukidhi masharti ya shirika la fedha la kimataifa – IMF, katika jitihada za mwisho za kuhakikisha kutolewa kwa fedha zaidi za uokoaji uchumi.

IMF katikati ya mwezi wa Juni ilieleza kutoridhishwa na bajeti ya awali ya nchi hiyo, ikisema imeshindwa kupanua wigo wa kodi kwa njia ya kimaendeleo zaidi.

Bajeti iliyorekebishwa iliidhinishwa siku moja baada ya waziri wa fedha Ishaq Dar, kuwasilisha kodi mpya na kupunguza matumizi.

“Muswada wa fedha umepitishwa,” spika wa bunge Raja Pervaiz Ashraf, alisema katika matangazo ya moja kwa moja ya televisheni siku ya Jumapili.

Huku akiba ya fedha haitoshi kugharamia uagizaji wa bidhaa kwa mwezi mmoja, Pakistan inakabiliwa na mzozo mkubwa wa malipo, ambao wachambuzi wanasema huenda ukaingia katika hali ya kutolipa deni ikiwa fedha za IMF hazitafanikiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG