Picha za waandamanaji, wengi wao wakiwa wamevalia nguo za rangi ya njano na kijani za bendera ya Brazil walifika kuonyesha uungaji mkono wao kwa Bolsonaro, na kusambaza ujumbe wao hadi kwenye vituo televisheni na mitandao ya kijamii.
Azma ya maandamano hayo bado haiku bayana na polisi hawakujibu haraka ombi la AP kutoa maoni.
Tangu Bolsonaro ashindwe na Lusi Inacio Lula da Silva katika uchaguzi wakuwania tena urais hapo Oktoba 30, wafuasi wake wamekuwa wakikusanyika kote nchini wakipinga kushindwa na kuyataka majeshi kuingilia kati.
Mapema Jumatatu, mamlaka ya uchaguzi nchini ilimpa da Silva na makamu wake hati rasmi ya kuidhinisha ushindi wao.