Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:18

Rais wa zamani Luiz Lula da Silva ashinda uchaguzi wa Brazil

Rais wa zamani wa Brazil na mgombea urais aliyeshinda Luiz Inacio Lula da Silva na mkewe Rosangela Lula da Silva, katika mkutano wa usiku wa uchaguzi siku ya marudio ya uchaguzi wa rais wa Brazil, huko Sao Paulo, Brazil, Oktoba 30, 2022. REUTERS

Rais wa zamani wa mrengo wa kushoto Luiz Inacio Lula da Silva alishinda uchaguzi wa Brazil ambao ulikuwa na ushindani mkali Jumapili, kulingana na mchambuzi wa data Datafolha, na kumnyima Jair Bolsonaro aliyepo madarakani muhula wa pili.

Shirika hilo la utafiti wa maoni liliitisha uchaguzi huo kwa asilimia 95 ya kura zilizohesabiwa katika nchi kubwa zaidi ya Amerika Kusini. Hesabu rasmi ilisimama kwenye asilimia 50.7 ya kura za Lula dhidi ya asilimia 49.3 ya Bolsonaro.

Idadi kubwa ya kura bado zimesalia kuhesabiwa katika jimbo la ngome ya Bolsonaro la Sao Paulo, lakini mpinzani wake wa mrengo wa kushoto alikuwa anasonga mbele katika duru ya pili iliyotawaliwa na shutuma kutoka kwa Chama cha Wafanyakazi cha Lula kwamba polisi walikandamiza kura katika baadhi ya mikoa.

Uchaguzi huo unatumika kama kura ya maoni kuhusu maono mawili tofauti na yanayopingana vikali kuhusu mustakabali wa Brazil.

XS
SM
MD
LG