Rais huyo alisema maandamano ya wafuasi wake yalikuwa matunda ya "ghadhabu na hisia ya ukosefu wa haki" kuhusu kura hiyo.
Hata hivyo, hakusema kuwa anapinga matokeo ya uchaguzi huo na kuidhinisha mkuu wake wa wafanyakazi wa Ikulu, Ciro Nogueira, kuanza mchakato wa mpito na wawakilishi wa Rais mteule wa mrengo wa kushoto Luiz Inacio Lula da Silva.
Ilimchukua Bolsonaro, mzalendo wa mrengo wa kulia, zaidi ya saa 44 kutoa maoni yake baada ya uchaguzi kuamuliwa na mamlaka ya uchaguzi, huku ucheleweshaji huo ukizua hofu kwamba angetaka kutilia shaka matokeo hayo waliopishana kwa kura chache.
Katika ukimya wake wafuasi wake walifunga barabara kuu kupinga kushindwa kwake, huku wengine wakitaka mapinduzi ya kijeshi kumzuia rais wa zamani Lula kurejea madarakani.
Vizuizi hivyo vya barabara kuu vimetatiza usambazaji wa mafuta, usambazaji wa maduka makubwa na usafirishaji wa nafaka kwenye bandari kuu, kulingana na vikundi vya sekta hiyo.