Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 17:57

Bolsonaro ashindwa kutetea kiti cha urais Brazil


Aliyekuwa rais Brazil Luiz Inacio Lula da Silva (kushoto) ambaye amemshinda rais wa sasa Jair Bolsonaro (kulia)
Aliyekuwa rais Brazil Luiz Inacio Lula da Silva (kushoto) ambaye amemshinda rais wa sasa Jair Bolsonaro (kulia)

Kiongozi wa mrengo wa kushoto nchini Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, ameshinda kura za urais.

Da Silva amemshinda rais aliyepo madarakani Jair Bolsonaro katika duru ya pili ya uchaguzi huo.

Bolsonaro, hajakiri kushindwa, na kuna ripoti kwamba huenda akakataa matokeo hayo.

Tume ya uchaguzi ya Brazil imemtangaza Lula, mwenye umri wa miaka 77 kuwa mshindi wa uchaguzi huo, baada ya kupata asilimia 50.9 ya kura. Bolsonaro amepata asilimia 49.1.

Da Silva alikuwa rais wa Brazil, anatarajiwa kuapishwa Januari 1.

Bolsomaro anakuwa rais wa kwanza aliye madarakani kushindwa katetea nafasi hiyo.

"Kufikia sasa, Bolsonaro hajanipigia simu kutambua kwamba nimemshinda, na sijui kama atafanya hivyo,” amesema Lula akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake waliokuwa wanasherekea ushindi wake katika mji wa San Paulo.

Hata hivyo, Lula amekuwa akipokea ujumbe wa pongezi kutoka kwa viongozi mbali mbali duniani, akiwemo Joe Biden wa Marekani, Vladimir Putin wa Russia, chansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Mwaka jana, Bolsonaro alisema wazi kwamba hatakubali matokeo ya uchaguzi wa urais endapo hatashinda, akidai kwamba mfumo wa upigaji kura kwa njia ya elektroniki unaweza kutumika kuiba kura.

XS
SM
MD
LG