Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 11:09

Wademokrat wakwamishwa kubadilisha sheria za uchaguzi na wanachama wao


Joe Manchin and Kyrsten Sinema wakitoka katika mkutano Bungeni, Washington, Marekani, Oktoba 21, 2021. REUTERS/Elizabeth Frantz
Joe Manchin and Kyrsten Sinema wakitoka katika mkutano Bungeni, Washington, Marekani, Oktoba 21, 2021. REUTERS/Elizabeth Frantz

Juhudi za mwaka mzima za Wademokrat hapa Marekani kutaka kubadilisha sheria za uchaguzi zimefeli baada ya maseneta wawili kukataa kukiunga mkono chama chao katika kubadilisha hoja ya kimkakati iliyowekwa na chama cha Republikan.

Baada ya saa kadhaa za majadiliano, baraza la senate lililogawanyika limepiga kura ambapo maseneta 49 dhidi ya 51 walipigia kura hoja ya kutaka mswaada huo kusonga mbele. Hoja hiyo ilihitaji kura 60.

Hoja hiyo iliyowasilishwa na kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Senate Chuck Schumer imeshindwa baada ya maseneta wawili wa Democrat Joe Manchin na Kyrsten Sinema kuungana na Warepublikan katika kuipinga.

Seneta anayeongoza Warepublican Mitch McConnell amesema kwamba jaribio la Wademocrat kubadilisha kanuni za bunge kwa kuanzisha mjadala mwingine ni zaidi ya kunyakua madaraka ya kisiasa.

"Nusu yetu upande huu walitumia miaka minne tu tulipokuwa tunaongoza Seneti na rais wetu alitaka tufanye wanachojaribu kufanya lakini walikataa. Hatutaharibu taasisi kwa maslahi ya muda mfupi.

Watetezi wa haki za kupiga kura wamesema kwamba mswaada huo ni muhimu wakati majimbo yanayoongozwa na Warepublican kote nchini yanaendelea kupitisha sheria zinazofanya kuwa vigumu kwa Wamarekani Weusi kupiga kura kwa kutaka vitambulisho maalum miongoni mwa mabadiliko mengine kwenye sheria za uchaguzi.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema kwamba amekasirishwa sana na hatua ya Seneti kushindwa kupitisha mswaada huo.

Hata hivyo, Biden amesema kwamba ataendelea kutafuta mbinu zingine za kutumia kila fursa aliyo nayo kutetea demokrasia.

XS
SM
MD
LG