Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 10:23

Rais Biden akabiliwa na maswali juu ya mustakbali wa demokrasia nchini


Polisi wakiimarisha ulinzi katika Bunge la Marekani baada ya ghasia za uvamizi wa uliofanywa na wafuasi wa Rais wa zamani Donald Trump, Januari 6, 2021 (AP Photo/John Minchillo)

Rais Joe Biden amekabiliwa na maswali kutoka kwa viongozi wa ulimwengu wenye wasiwasi, ambayo hajawahi kufikiria kuwa atayasikia.

“Je Marekani itakuwa shwari?” wanauliza. “Je vipi kuhusu demokrasia nchini Marekani?”

Wakati Biden amejaribu kutoa uhakikisho kwa washirika wa Marekani, amefanya hilo tu katika baadhi ya nyakati akisisitiza ukubwa wa tishio dhidi ya demokrasia kutokana na ghasia za uvamizi wa Bunge la Marekani Januari 6 na kukaririwa kwa uongo unaoenezwa na mtu aliyemshinda katika uchaguzi, Donald Trump, kuwa uchaguzi wa 2020 uligubikwa na wizi.

Rais bado hajajadili wasiwasi wa kweli kuhusu kuongezeka kwa wenye masikitiko kwa wale waliofanya ghasia za uvamizi ambao wamechaguliwa katika uchaguzi wa mitaa na mabadiliko yanayofanywa na Warepublikan katika sheria za uchaguzi katika majimbo kadhaa.

Hivi sasa, wakati kumbukumbu ya tukio lile ovu likikaribia, rais Mdemokrat anasisitizwa kupanga upya vipaumbele na kutumia mamlaka ya ofisi yake kushinikiza sheria ya haki ya uchaguzi ambayo wanaoziafiki wanasema itakuwa njia mwaafaka pekee ya kukabiliana kwa haraka na vitisho vinavyojitokeza dhidi ya mchakato wa demokrasia.

Ugumu wa muelekeo anauchukua Biden unaonyesha anavyojaribu kutengeneza uwiano wa mahitaji muhimu ya Wamarekani ili kupiga hatua katika mambo yanayovuma zaidi ya janga la virusi vya corona na uchumi na yale ambayo hayavumi, lakini yanaumuhimu sawa, suala la kuendeleza uaminifu katika uchaguzi na serikali.

Rais anampango wa kutoa hotuba Januari 6 ikiangazia juu ya kuendeleza demokrasia – haki za kupiga kura hazitakuwa sehemu ya hotuba hiyo lakini itakuwa ni maudhui ya hotuba nyingine siku za karibuni, wasaidizi wa White House wamesema.

Katika hotuba yake ya ufunguzi hivi karibuni katika Chuo Kikuu cha Jimbo la South Carolina, kauli ya Biden juu ya umuhimu wa kuwepo sheria ya haki za kupiga kura ilionyesha kuongeza dharura ya kuwepo.

“Sijawahi kuona kitu kama juhudi la shambulizi dhidi ya haki ya kupiga kura. Kamwe,” Biden alisema, akiongeza, “Huu uovu mpya uliochanganyika na ukandamizaji wa upigaji kura na ukandamizaji wa uchaguzi, siyo Umarekani, ni dhidi ya demokrasia, na inasikitisha, haijawahi kutokea tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe.”

Na dunia inalitambua hilo. Mshauri wa usalama wa taifa wa Biden, Jake Sullivan, pia amesema kuwa ghasia za uvamizi katika Bunge la Marekani imebadilisha maoni ya nchi nyingi walivyokuwa waniona Marekani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG