Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 20:20

Miji mikuu Marekani yajiandaa kuwadhibiti waandamanaji wenye silaha


Maua yamewekwa katika uzio wa waya wenye makali unaolizunguka Bunge la Marekani ikiwa ni hatua ya kuimarisha ulinzi, Januari 15, 2021 in Washington, DC baada ya uvamizi uliofanywa na wafuasi wa Rais Trump.

Ulinzi uko katika hali ya kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa kwa miaka mingi huku baadhi ya sehemu za mji wa Washington zimefungwa kabisa.

Wakati huohuo maafisa wa usalama wa Marekani wanachukuwa tahadhari dhidi ya maandamano ya wafuasi wa Trump katika miji mikuu ya majimbo yote 50 kipindi cha wikiendi.

Pia tayari kumewekwa vizuizi na Walinzi wa Kitaifa kupelekwa maeneo hayo ili kuzuia aina yoyote ya uvunjifu wa amani kama ule uliolitikisa taifa Januari 6.

Walinzi wa Kitaifa wakifanya doria ndani ya uzio uliowekwa kuzunguka Bunge la Marekani
Walinzi wa Kitaifa wakifanya doria ndani ya uzio uliowekwa kuzunguka Bunge la Marekani

Idara ya Upelelezi wa Jinai FBI imetahadharisha idara za polisi juu ya kuwepo uwezekano wa waandamanaji wenye silaha nje ya majengo ya bunge katika majimbo yote 50 kuanzia Jumamosi hadi siku ya kuapishwa Rais mteule Joe Biden Januari 20, yaliochochewa na wafuasi wa Rais Donald Trump wanaoamini madai yake ya uongo ya wizi wa kura.

Michigan, Virginia, Wiscosin, Pennsylvania na Washington ni kati ya majimbo yaliyoitisha walinzi wa kitaifa kuimarisha usalama.

Texas ilifunga Bunge lake hadi kumalizika sherehe za kuapishwa rais. Steve McCraw, mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Umma ya Texas, amesema katika taarifa yake Ijumaa jioni kuwa ripoti za kiintelijensia zinaashiria “vikundi vyenye misimamo mkali vinavyo kusudia kuvunja amani” vinaweza kutumia fursa ya maandamano ya watu wenye silaha yaliyopangwa huko Austin “kutekeleza vitendo vya uhalifu.”

Mjini Washington, maafisa wamemkamata mtu mmoja mkazi wa Virginia aliyekuwa anajaribu kupita kizuizi kilichowekwa na Polisi wa Bunge la Marekani akitumia vitambulisho bandia vya sherehe za kuapishwa rais, akiwa na bunduki iliyokuwa na risasi na risasi nyingine zaidi ya 500, Kituo cha televisheni cha CNN na gazeti la New York Times yameripoti Jumamosi, wakinukuu ripoti ya polisi na vyanzo vya vyombo vya usalama.

Mtu huyo amefunguliwa mashtaka ya makosa ya uhalifu matano, ikiwemo kumiliki silaha isiyokuwa na kibali na risasi, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Maafisa wa polisi wa bunge la Marekani hawakupatikana kutoa maelezo juu ya habari hizi.

Juhudi hizi za kuimarisha ulinzi zinafuatia uvamizi uliosababisha ghasia uliotokea Januari 6 katika Bunge la Marekani ukitekelezwa na mchanganyiko wa wafuasi wa Trump na wale wenye mismamo mkali.

Wafuasi wa Rais Trump wakijaribu kuvuka kwa kutumia mabavu kizuizi kilichowekwa na polisi katika eneo la Bunge la Marekania mjini Washington, Jumatano Januari 06, 2021.
Wafuasi wa Rais Trump wakijaribu kuvuka kwa kutumia mabavu kizuizi kilichowekwa na polisi katika eneo la Bunge la Marekania mjini Washington, Jumatano Januari 06, 2021.

Baadhi yao walikuwa na mipango ya kuwateka nyara wabunge na wakipaza sauti makamu wa rais Mike Pence auwawe wakati akiongoza zoezi la kurasmisha ushindi wa Biden baada ya uchaguzi uliofanyika mwezi Novemba.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG