Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 23:13

Rais mteule wa Marekani Biden amezindua mpango wa auheni wa COVID-19


Rais mteule Joe Biden akizindua mpango wa auheni ya COVID huko Wilmington, Delaware, Januari 14, 2021

Mpango wa Biden unajumuisha mzunguko mpya wa malipo ya moja kwa moja kwa kaya za Marekani, fedha za kuhamasisha shule kufunguliwa kwa usalama na kuongeza program ya chanjo kitaifa

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amezindua Alhamis mpango wa majibu ya virusi vya Corona ambao ni pamoja na kuongeza kiwango cha chanjo na kusaidia kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na janga hilo.

The American Rescue Plan utazungumzia kwa kina masuala tofauti, muingiliano usio sawa wa kizazi ambao umezidi kuwa mbaya kufuatia COVID-19, taarifa kutoka timu ya mpito ilisema.

Mpango wa Biden, unajumuisha mzunguko mpya wa malipo ya moja kwa moja kwa kaya za Marekani, fedha za kuhamasisha shule kufunguliwa kwa usalama na kuongeza program ya chanjo kitaifa.

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden
Rais mteule wa Marekani, Joe Biden

Pia kutoa auheni kwa biashara ndogo ndogo, haswa zile zinazomilikiwa na wajasiriamali weusi, pia ilifafanuliwa katika mpango huo.

Mpango wa American Rescue Plan wa Rais mteule Joe Biden unagharimu dola bilioni 1.9, lakini unaweza kutekelezwa na utaokoa uchumi wa Marekani na kuanza kukabiliana na virusi, taarifa hiyo ilieleza.

Biden ameweka lengo la kutoa dozi za chanjo milioni 100 katika siku 100 za kwanza, baada ya kuchukua madaraka hapo januari 20, na mpango wake unatarajiwa kujumuisha fedha za kupanua kampeni ya chanjo.

XS
SM
MD
LG