Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 12:39

Zaidi ya wafuasi 170 wa Rais Trump waliovamia Congress wametambuliwa


Trump supporters try to break through a police barrier, Jan. 6, 2021, at the Capitol in Washington.
Trump supporters try to break through a police barrier, Jan. 6, 2021, at the Capitol in Washington.

Waendesha mashtaka wa Marekani wamesema Jumanne wamekwisha watambua zaidi ya watu 170 ambapo kuna uwezekano wakafunguliwa mashtaka.

Hatua hii ni kufuatia uhalifu uliofanywa na wafuasi wa Rais Trump waliovamia jengo la Bunge la Marekani wiki iliyopita.

Wamesema idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kwa mamia katika wiki zijazo wakati upelelezi mkubwa wa nchi nzima unaendelea kuwasaka waandamanaji hao wanaomuunga mkono Trump.

Michael Sherwin, kaimu mwanasheria msaidizi wa Washington DC amewaambia wana habari kuwa zaidi ya watu 70 wameshtakiwa hadi hivi sasa hapa Washington.

Pia waendesha mashtaka wanataka kuwasilisha mashtaka zaidi dhidi ya watu wengine 100.

Wakati huo huo kiongozi wa Wademocrat walio wachache katika Baraza la Seneti, Chuck Schummer amesema wafuasi wa Rais Trump ambao walivamia na kushambulia jengo la Capitol Hill ni vyema wapigwe marufuku kusafiri kwa ndege.

XS
SM
MD
LG