Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 16:03

Bunge larasmisha ushindi wa Joe Biden kuwa Rais wa 46 Marekani


Makamu Rais Mike Pence (kushoto) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi wakijiandaa kutoa tamko la kurasmisha ushindi wa Biden katika kikao cha pamoja cha Bunge Alhamisi alfajiri Januari 7, 2021.J. Scott Applewhite/Pool via REUTERS
Makamu Rais Mike Pence (kushoto) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi wakijiandaa kutoa tamko la kurasmisha ushindi wa Biden katika kikao cha pamoja cha Bunge Alhamisi alfajiri Januari 7, 2021.J. Scott Applewhite/Pool via REUTERS

Bunge la Marekani Alhamisi alfajiri lilirasmisha ushindi wa Mdemokrat Joe Biden kama rais wa 46 Marekani baada ya shughuli hiyo kucheleweshwa saa kadhaa kufuatia uvamizi wa majengo ya bunge na wafuasi wa Rais Donald Trump Jumatano jioni.

Uvamizi huo umetokea wakati wabunge wa mabaraza mawili walipoanza utaratibu wa kurasmisha ushindi wa Joe Biden.

Wabunge walilazimika kuondolewa ndani ya bunge na kuwekwa mahali salama hadi maafisa wa usalama walipofanikiwa kuondoa wavamizi ndani ya majengo ya bunge.

Licha ya mamia ya wafuasi wa Trump kuvamia bunge na kupambana na maafisa wa usalama Wabunge wa vyama vyote viwili walirudi tena Jumatano usiku na kuendelea kupokea hesabu za kura za majimbo na kurasmisha matokeo ya wajumbe wa uchaguzi kwa ushindi wa kura za wajumbe 306 kwa 232.

Makamu Rais Mike Pence na Spika Nancy Pelosi wakiongoza kikao cha pamoja cha Bunge kurasmisha ushindi wa Joe Biden, Alhamisi alfajiri, Januari 7, 2021.
Makamu Rais Mike Pence na Spika Nancy Pelosi wakiongoza kikao cha pamoja cha Bunge kurasmisha ushindi wa Joe Biden, Alhamisi alfajiri, Januari 7, 2021.

Wajumbe kadha katika mabaraza ya seneti na wawakilishi walijitoa katika juhudi za kupinga uthibitishaji wa matokeo baada ya vurugu zilizotokea Jumatano.

Makamu Rais Mike Pence alikuwa wa kwanza kuzungumza katika kikao hicho cha pamoja cha mabaraza yote mawili kama rais wa Baraza la Seneti baada ya kuahirishwa kwa muda.

Makamu wa rais Pence alisema : "Leo ilikuwa siku ya kiza katika historia ya bunge la Marekani. Lakini ninatoa shukurani kwa juhudi za haraka za polisi wa bunge wakishirikiana na polisi wa serikali kuu na wale wa hapa mjini kukomesha ghasia hizo."

Viongozi wa vyama vyote viwili na wabunge kwa ujumla wamelaani uvamizi huo ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia ya hapa Marekani.

Naye Rais Mteule Joe Biden akiwa Delaware nyumbani kwake alilihutubia taifa na kulaani ghasia zilizo tokea na kusema ameshtushwa na kuskitishwa na tukio hilo.

Biden alisema : "Kuvamia jengo la bunge, kuvunja madirisha kukalia ofisi za wabunge. Kuingia ndani ya baraza la seneti na kuharibu madawati na vitu vya maafisa wa bunge. Kutishia usalama wa watu waliochaguliwa. Hayo si malamamiko ya amani. Huo ni uasi."

Wanasiasa, wachambuzi na sehemu kubwa ya Wamarekani wanamlaumu rais kwa kuwachochea wafuasi wake na kusababisha ghasia hizo. Na Akizungumza katika ujumbe wa vídeo baada ya ghasia hizo na wito wa Biden, Trump alirudia madai yake ya kuibiwa kura na kuwataka wafuasi wake warudi nyumbani.

Rais Trump alisema : "Ulikuwa ni ushindi mkubwa wakati wa uchaguzi na kila mtu anafahamu hilo, hasa wale wa upande wa upnzani wetu. Lakini hivi sasa munabidi kurudi nyumbani."

Kampuni za mitandao ya kijami ya Twitter na Facebook kwa mara ya kwanza zilifunga ukurasa wa Trump kwa siku moja kwa madai ya kukiuka sera zao.

Viongozi mbali mbali wa Dunia wameshtushwa na matukio ya Jumatano na kulaani uvamizi wa bunge la Marekani.

Na baada ya wabunge kuidhinisha ushindi wa Biden usiku wa manane wabunge 17 wa Baraza la Wawakilishi walimpongeza Makamu Rais na kumtaka kutangaza kifungu cha 25 cha kumondoa Trump madarakani , hatua ambayo huenda isifanyike wiki mbili kabla ya muda wake madarakani kumalizika.

Aziz Huq Mhadhir wa Chuo Kikuu cha Chicago anasema itakuwa vigumu kutumia kifungu hicho cha Katiba.

Aziz Huq anasema : Kifungu cha 25 kwa hakika ni kuhusu kutoweza kufanya kazi, na uwezo wa kutumikia madaraka kiafya au kinguvu. Haihusiana ni uwezo wa kiakili wa rais. Kwa hivyo ni muhali kwa Trump kuondolewa madarakani kwani Biden ataapishwa hapo Januari 20 kua rais wa 46 wa Marekani."

Matukio hayo yalipokuwa yanaendelea habari zilitokea kwamba Warepublican wanapoteza udhibiti wa Baraza la Seneti kutokana na ushindi wa Jon Ossoef, aliyekua anapigania kiti kimoja cha baraza la Senet katika jimbo la Georgia.

Ushindi huo ni mkubwa sana kwa chama cha Demokratik kwani hivi sasa Wademokrat kwa mara ya kwanza tangu awamu ya kwanza ya utawala wa Barack Obama watashikilia udhibiti wa mabaraza mawili ya bunge na White House.

XS
SM
MD
LG