Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:25

Trump na Biden wapiga kampeni katika uchaguzi wa duru ya pili wa seneti Georgia


Seneta Kelly Loeffler, kushoto Mrepublikan na mpinzani wake Mdemokrat Raphael Warnock katika mdahalo Dec. 6, 2020, jijini Atlanta.
Seneta Kelly Loeffler, kushoto Mrepublikan na mpinzani wake Mdemokrat Raphael Warnock katika mdahalo Dec. 6, 2020, jijini Atlanta.

Uchaguzi wa duru ya pili wa viti viwili vya seneti huko katika jimbo la Georgia unafanyika Jumanne na utaamua ikiwa Warepublican au Wademokrat watachukua udhibiti kwenye baraza la Seneti la Marekani na kubadili kwa kasi utekelezaji wa sera katika nusu ya kwanza ya muhula wa miaka minne wa Rais mteule Joe Biden katika Ikulu ya Marekani.

Huku uchaguzi ukiwa na umuhimu mkubwa wote Biden na Rais anayemaliza muda wake Donald Trump wamefanya mikutano ya kampeni ya dakika za mwisho katika jimbo hilo Jumatatu, hata wakati Trump akiendelea na malalamiko yake dhidi ya maafisa wa uchaguzi wa Georgia kwa kukataa kubadili matokeo ya uchaguzi ambayo alishindwa kwa kura chache na Joe Biden katika jimbo hilo katika uchaguzi wa Novemba 3.

Rais anayeingia madarakani amefanya kampeni huko Atlanta, jiji kubwa zaidi la Georgia, kwa Wademokrat wawili, Jon Ossoff, mtayarishaji wa filam , na Mchungaji Raphael Warnock, mchungaji wa kanisa la Baptist. Wakati huo huo, rais Trump amefanya kampeni katika eneo kubwa la Warepublican huko Dalton kaskazini mwa jimbo hilo ajili ya Seneta David Perdue, ambaye wakati fulani alikuwa mfanyabiashara mkubwa anayekabiliana na Ossoff, na kwa Seneta Kelly Loeffler, mmoja wa seneta tajiri zaidi Marekani ambaye anakabiliana na mchungaji Warnock.

Imaetayarishwa na Sunday Shomari, VOA ,Washington DC

XS
SM
MD
LG