Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 22:49

Baadhi ya Warepublikan kupinga kuidhinishwa kwa ushindi wa Biden


Jengo la bunge la Marekani.
Jengo la bunge la Marekani.

Zaidi ya wabunge 100 wa chama cha republikan wakishirikiana na darzeni ya maseneta kutoka chama hicho wanasema kuwa Jumatano watashiriki kwenye juhudi za kujaribu kupinga kutiwa saini ushindi wa kura za wajumbe wa majimbo kwamba rais mteule Joe Biden alimshinda rais Donald Trump kwenye uchaguzi wa Novemba.

Hatua hiyo ya kuidhinisha Biden kuwa na kura 306 dhidi ya 232 za Trump ndiyo hatua ya mwisho kuelekea sherehe za kuapishwa kwa Biden kama rais wa 46 hapo Januari 20. Ushindi huo ni lazima uidhinishwe na mabunge yote mawili kabla ya Biden kuapishwa.

Lakini Wanademokrat wanaodhibiti Bunge kwa wingi mdogo wana hakika watathibitisha ushindi wa Biden, wakati katika baraza la seneti walipo wachache pamoja na Warepublican walio wengi ambao baadhi yao wamekiri ushindi wa Biden, wana uwezekano wa kufanya vivyo hivyo kwenye baraza hilo.

Kwa wiki kadhaa sasa tangu zoezi hilo kumalizika, Trump amekuwa akidai kuwa uchaguzi uliibwa, bila kuwa na ushahidi wowote, na iwapo Biden ataidhinishwa, basi Trump atakuwa rais wa tano katika historia ya Marekani ya miaka 245 kushindwa kuingia uongozini kwa muhula wa pili.

Kupitia video fupi aliotuma kwa njia ya twitter, Trump ameomba wafuasi wake kujitokeza kwa wingi Jumatano hapa Washington DC ili kupinga kuidhinishwa kwa Biden kama Rais wa Marekani akisema linaweza kuwa tukio kubwa kabisa katika historia ya mji huo.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washington DC


XS
SM
MD
LG