Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 21:01

Wademokrat washinda kiti kimoja cha Seneti Georgia; Congress yaingiliwa na wafuasi wa Trump


Jon Ossoff kushoto na Raphael Warnock wakiwa katika Kampeni ya chama cha Demokratik.
Jon Ossoff kushoto na Raphael Warnock wakiwa katika Kampeni ya chama cha Demokratik.

Lakini wakati matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa Seneti Georgia ukisubiriwa makao makuu ya Congress, Washington, yailingiliwa na wafuasi wa Trump wanaopinga matokeo ya urais ambayo yalipangwa kurasmishwa bungeni leo.

Ushindi huo kutokana na matokeo ya awali unakaribia kukipatia chama hicho udhibiti wa Baraza la Senati na hivyo kumpatia madaraka Rais mteule Joe Biden uwezo wa kutekeleza malengo yake ya kisiasa atakapo chukuwa madaraka hapo Januari 20.

Ushindi wa Mchungaji Raphael Warnock uliotangazwa na vyombo vya habari vya Marekani dhidi ya mpinzani wake Seneta Kelly Loeffler mapema Jumatano, unafuatia kampeni kali na kabambe ya wiki tisa kaika jimbo hlo ambalo kwa miongo kadhaa sasa linashikiliwa na Warepublican.

Kura zikiwa karibu zote zimehesabiwa Warnock ambaye anakuwa Seneta wa kwanza Mmarekani mweusi wa jimbo hilo anaongoza kwa zaidi ya kura elfu 40. akiwahutubia wafuasi wake jana usiku aliahidi kufanya kazi kwa maslahi ya wa georgia wote.

Mchungaji Raphael Warnock akiongea na wafuasi wake Januari 5, 2021 in Marietta, Georgia.
Mchungaji Raphael Warnock akiongea na wafuasi wake Januari 5, 2021 in Marietta, Georgia.

Mchungaji Warnock anaeleza : "Georgia, ni heshima kubwa kwangu kutokana na imani yenu mliyonipatia. Na nina ahidi hii leo kwamba nina kwenda kwenye Baraza la Seneti ili kufanya kazi kwa wa Georgia wote bila ya kujali nani kanipigia kura."

Warnock anasema ana matumiani ushindi wake ambao hakuna aliyetarajia utakuwa mfano kwa vijana kwamba kila kitu kinawezekana kufikia ndoto ya Marekani.

Warnock anaongeza kuwa : "Tuliambiwa hatuwezi kushinda katika uchaguzi huu lakini leo usiku tumedhihirisha kwamba tukiwa na matumaini na kufanya kazi kwa bidi na kushirikiana na watu wote basi chechote kile kinawezekana."

Katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa pili Mdemokrat Jon Ossoff mwandishi habari anaongoza kwa zaidi ya kura elfu 12 dhidi ya Seneta Mrepublican David Perdue aliyekua anagombania mhula wake wa pili wa miaka 6.

Jon Ossoff (kushoto), Raphael Warnock (Kulia) na Rais mteule Joe Biden (katikati) wakiwa katika kampeni uwanja wa Center Parc Atlanta, Georgia, on January 4, 2021.
Jon Ossoff (kushoto), Raphael Warnock (Kulia) na Rais mteule Joe Biden (katikati) wakiwa katika kampeni uwanja wa Center Parc Atlanta, Georgia, on January 4, 2021.

Ikiwa Warepublican watashindwa katika kupigania kiti hicho cha pili basi hiyo itakua pigo la pili kwa hii leo kwa rais Donald Trump na warepublican anaopinga matoeo ya uchaguzi wa rais ambayo yanathibitishwa rasmi hii leo na bunge la Marekani. Wafuasi wa Trump wamekusanyika hapa mjini washington tangu jana kwa maandamano hii leo kudai kwamba kulikua na wizi wa kura akati wa uchaguzi wa Novemba.

Laura Uvualle mfuasi wa Trump anasema kunahaja ya kurudia uchaguzi huo, akisema : "Ikiwa wanataka basi kufanye uchaguzi mwengine wacha tupige kura kwa mara nyingine, lakini bila ya mashini zilizokuwa zina hesabu kura za uwongo na kufanya mambo yasio sawa. Donald Trump alishinda uchaguzi."

Tukielekea kwenye uchaguzi wa jana Wademokrat walikuwa na viti 48 dhidi ya 50 vya Warepublican kwenye Baraza la Seneti.

Hivyo kutokana na ushindi wa Warnock na uwezekano wa Ossoff kupata ushindi Wademokrat watakuwa na viti sawa na Warepublican 50 kwa 50 na hapo kumpatia nafasi Makamu Rais mteule Kamala Harris ambaye anakuwa pia rais wa baraza hilo kuongoza kazi za baraza akiamua na kupiga kura kuwapatia wingi Wademokrat.

Wademokrat tayari wana wingi mdogo kwenye baraza la wawakilishi. Hivyo kutokana na kuchukua udhibiti wa mabaraza yote mawili Biden ataweza kupendekeza mageuzi muhimu katika ajenda yake ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za afya, kurudisha sheria za kudhibiti mazingira zilzondolewa mnamo miaka minne ya utawala wa Trump na kujaribu pia kulegeza sheria za uhamiaji.

Lakini pindi Warepublican watachukua tena udhibiti wa baraza la Senet basi hali ya kisiasa ya Biden itaweza kua ngumu na huwenda akalazimika kufanya majadiliano ya mara kwa mara na wabunge wa Republican juu ya masuala tete.

XS
SM
MD
LG