Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 01:19

Maduro asheherekea ushindi uliotangazwa na chama cha kitaifa cha uchaguzi Venezuela


Rais Nicolás Maduro wa Venezuela
Rais Nicolás Maduro wa Venezuela

Matokeo hayo ni kikwazo kwa viongozi wa upinzani waliorejea kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kususia kura za urais mwaka 2018 na za ubunge mwaka 2020 wakisema kura ya haki haikuwezekana kutokana na kuibiwa kura na kutishwa kutoka magenge ya vurugu yanayomtii Maduro

Baraza la taifa la uchaguzi la Venezuela (CNE) limekipa ushindi chama tawala cha kisoshalist katika nyadhifa 20 za ugavana na tatu kwa wanasiasa wa upinzani katika tangazo la awali siku ya Jumatatu kufuatia uchaguzi wa mitaa na kikanda.

Muda mfupi baada ya matokeo ya kwanza kuchapishwa Rais wa mrengo wa kushoto Nicolas Maduro alisheherekea ushindi wa serikali. Ushindi unavutia, Maduro alisema, akiwa amezungukwa na wafuasi, akiongeza kuwa ushindi mzuri lazima ushangiliwe.

Matokeo hayo ni kikwazo kwa viongozi wa upinzani waliorejea kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kususia kura za urais mwaka 2018, na za ubunge mwaka 2020 wakisema kuwa kura ya haki haikuwezekana, kutokana na kuibiwa kura na kutishwa kutoka magenge ya vurugu yanayomtii Maduro.

Mmoja wa wapiga kura Venezuela
Mmoja wa wapiga kura Venezuela

Mwaka huu wanasiasa wa upinzani waliamua kushiriki katika uchaguzi huo, huku wakichoshwa na kushindwa kwa vikwazo vya Marekani kumfurusha Maduro, pamoja na kutiwa moyo na uwepo wa waangalizi wa uchaguzi kutoka umoja wa ulaya.

Ni asilimia 41.8 pekee ya wapiga kura waliojiandikisha walijitokeza kupiga kura siku ya Jumapili, sawa na watu wapatao milioni 8.1 mamlaka ya juu ya uchaguzi katika nchi hiyo ya Amerika kusini ilisema.

XS
SM
MD
LG